Machapisho

HALMASHAURI YA MONDULI YATUA HALMASHAURI YA JIJI LA DAR KUJIFUNZA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam. TIMU ya wataalamu kutoka Halmashauri ya wilaya ya Monduli mkoani Arusha ikiongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Happiness Laizer imefika katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kwa lengo kujifunza jinsi ya ukusanyaji wa mapato. Timu hiyo imepokelewa na mwenyeji wao Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji hilo ndugu Elihuruma Mabelya ambapo katika mazungumzo yake aliwaeleza wataalamu hao kuwa ufanisi wa ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam unachangiwa na ushirikiano wa watumishi katika kanda maalum za ukusanyaji mapato. Amesema uanzishwaji wa kanda hizo, umewezesha kuwasogezea wananchi huduma mbalimbali katika maeneo yao hali iliyochangia kuwapunguzia umbali wa kufuata huduma zikiwemo vibali mbalimbali, leseni n.k makao makuu ya Halmashauri.

SOMO LA LEO KUTOKA RSA TANZANIA

Picha
KWAmujibu wa kifungu cha 5(1)(e) cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) na Kanuni za LATRA za Usajili na Uthibitishaji Madereva na Wahudumu wa Mabasi (THE LAND TRANSPORT REGULATORY AUTHORITY (CERTIFICATION OF COMMERCIAL VEHICLE DRIVERS AND REGISTRATION OF CREW) REGULATIONS)) 2020, Dereva aliyesajiliwa na Kuthibitishwa na LATRA ana wajibu ufuatao kama sehemu ya masharti ya Kuthibitishwa kwake:  1. Kuzingatia mwendo kikomo (speed limits) uliowekwa barabarani kwa mujibu wa sheria; 2. Kutoendesha gari huku akiwa amelewa pombe au madawa ya kulevya; 3. Kuheshimu amri halali ya askari polisi au maafisa wa LATRA; 4. Kuendesha gari akiwa na leseni hai na cheti cha uthibitishwaji Kwa dereva anayeendesha gari la abiria, anatakiwa kuzingatia masharti yafuatayo ya ziada, kwa mujibu wa kanuni ya 10(2) ya kanuni tajwa hapo juu:  1. Kutopakia abiria Zaidi ya uwezo wa gari kama ulivyoandikwa kwenye cheti cha usajili wa/au leseni ya, gari; 2. Kuhakikisha milango imefungwa kab...

WAZIRI MKUU AKAGUA UKARABATI WA SOKO LA MAJENGO NA KUELEKEZA UKAMILIKE

Picha
Na Lubango Mleka, Dodoma WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ametembelea Soko la Majengo jijini Dodoma na kukagua maendeleo ya ukarabati wa soko hilo, ambapo amemuelekeza mkandarasi Kampuni ya Azhar Construction kukamilisha ukarabati huo ifikapo Mwezi Februari 2026 ili wafanyabiashara waanze kulitumia. Katika kuhakikisha maelekezo yake yanatekelezwa, Dkt. Mwigulu amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Dkt. Frederick Sagamiko kufanya makubaliano ya kimaandishi na mkandarasi huyo kuwa, hakutakuwa na nyongeza ya muda wa ukarabati wa soko hilo ifikapo Mwezi Februari, 2026. “Serikali inataka ukarabati wa Soko ukamilike kwa wakati ili kukidhi mahitaji ya wakazi wa Jiji la Dodoma, ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira wezeshi ya kuendelea kukuza uchumi wa wafanyabiashara,” Dkt. Nchemba amesisitiza. Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe akimkaribisha Mhe. Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa ukarabati wa ...

GRUMETI FUND YAWEZESHA SAFARI KWA VIJANA WAWILI KUJIFUNZA NAMNA BORA YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NCHINI TAIWAN

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Serengeti. SHIRIKA la Grumeti Fund kupitia Idara ya Maendeleo ya jamii, kituo cha Mazingira, limefadhili safari ya vijana wawili kutoka katika Shule za Sekondari Issenye na Natta za Wilayani Serengeti kwenda nchini Taiwan kwa ajili ya programu maalum ya kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu namna bora za utunzaji na uhifadhi wa mazingira.  Msimamizi wa Kituo cha Mazingira Bw. Laurian Kahatano amebainisha kuwa, Flora Nyaboko Gesimba, Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Natta na Mkazi wa Kijiji cha Maburi pamoja na Cosmas Godfrey Kitena, Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Issenye na Mkazi wa Kijiji cha Singisi wamepata ufadhili wa safari hiyo baada ya kuibuka washindi katika shindano la uandishi wa i insha (Essay) lililohusisha wanafunzi 32 kutoka katika shule 16 zilizopo kwenye program ya Elimu ya Mazingira inayoendeshwa kwenye kituo chetu cha Mazingira (EEC). "Hivi karibu tuliendesha mdahalo wa utunzi wa insha, katika shule zote 16 ambapo wanafunzi walipewa ...

WANAWAKE NKINGA HOSPITALI WAZINDUA KIKUNDI CHA KUSAIDIANA

Picha
Na Lubango Mleka, Nkinga - Igunga. WANAWAKE watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Nkinga jana Disemba 11, 2025 wamezindua rasmi kikundi chenye lengo la kusaidiana katika changamoto mbalimbali za kimaisha. Kikundi hicho kilichopewa jina la Nkinga Super Women Group kimezinduliwa katika Kikao cha kwanza cha Kufunga Mwaka, ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ndg.Victor Ntundwe alikuwa ndiye mgeni rasmi. "Ninawapongeza kwa kuunganisha nguvu ya pamoja katika kukabiliana na changamoto zenu, Siku zote Umoja ni nguvu, Uongozi wa hospitali unawathamini sana kwa jinsi mnavyoongoza wafanyakazi wengine kwa nidhamu, weledi na kuwa vinara wa huduma kwa mteja" amesema Mkurugenzi Ntundwe katika hotuba yake Bi.Epifania Nyaki ni mwenyekiti wa Umoja huo amesema, kuanzishwa kwa Umoja huo ni matokeo ya mawazo katika sherehe ya Siku ya Wanawake Duniani Machi, 2024 baada ya kushikwa mkono na Mkurugenzi wa Hospitali, na ndipo January 2025 kikundi hicho kikaanza rasmi. Ameongeza, kwasasa kikundi hich...

TANZIA

Picha
  SPIKA WA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. MUSSA AZZAN ZUNGU (MB) ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MBUNGE WA PERAMIHO MHE. JENISTA JOAKIM MHAGAMA KILICHOTOKEA LEO 11,DESEMBA,2025 JIJINI DODOMA.

AMNESTY INTERNATIONAL YALISHUTUMU KUNDI LA HAMAS

Picha
SHIRIKA la Amnesty International limeishtumu Hamas na makundi mengine ya wapiganaji wa Kipalestina kwa mara ya kwanza kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, ikiwemo mauwaji, wakati na baada ya shambulio la Oktoba 7, 2023 lililochochea vita vya Gaza. #HamasIsISIS ##palestine #AmnestyInternational

UJUMBE WA LEO KUTOKA RSA TANZANIA

Picha
   NDANI ya Jiji la Dar es Salaam au kwengineko ukiendesha kwa mwendo wa wastani wa kati ya 50-60Kph kwenye Zebra yoyote utaweza kusimama na kuwapisha wavukaji wavuke, ila spidi ikizidi hapo sio rahisi kusimama hasa mwenda kwa miguu anapotokea ghafla.  Hata hivyo, Jizoeshe Kusimama kwenye kila zebra kupisha watu wavuke, maana hata wewe ni mwenda kwa miguu ukitoka kwenye usukani.  Usiposimama kuwapisha, hawatakuwa na mahala pengine salama pa kuvuka zaidi ya kuhatarisha maisha yao.  Hivyo jambo la kwanza ondoa ile kasumba au mtazamo kuwa *Aagh wasumbufu hawa*, kwakuwa hata wao hao unaowaona kero wana haki ya kutumia barabara. Ni tofauti ya kipato tu au mazingira ya wakati huo ndio yamewafanya kwenda kwa miguu.  Na jinsi miji inavyozidi kukua ndivyo idadi ya watu inavyoongezeka huku kukiwa na miundo mbinu michache sana ya waenda kwa miguu, tegemea idadi kubwa ya waenda kwa miguu kila kwenye zebra. Hivyo kuwa mwenda kwa miguu sio dhambi.  Hii ndio sababu k...

AMUUA MWANAYE KWA KIPIGO

Picha
Na Mwandishi Wetu, Mbeya. MWANAMKE Mmoja  aitwaye ,Marry Timotheo mkazi wa kijiji cha Garijembe kata ya Tembela Wilaya ya Mbeya anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga na kitu kizito kichwani mtoto wake, Scola Mwaba(10)kwa madai ya kuzidi utukutu kisha mwili wake kutupa shamba lilo karibu na nyumbani anakoishi . Akizungumzia tukio hilo Desemba 10,2025 Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema marehemu Scola alikuwa Mwanafunzi wa Darasa la Nne shule ya Msingi Ngonde wilaya ya Mbeya.  Kuzaga amesema kuwa tukio hilo limetokea Desemba 9,2025 ,majira ya saa 6.30 mchana katika Kijiji cha Garijembe ,Kata na Tarafa ya Tembela  Wilaya ya Mbeya. "Mama wa marehemu alimshambulia kwa kitu kizito kichwani  mtoto wake kwa madai ya kuzidi utukutu kisha mwili wake kutupa jirani na shamba la nyumba anakoishi "amesema Kamanda Kuzaga.  Aidha Kuzaga ameeleza kuwa pia licha ya  kumshikilia mama wa marehemu ,pia  jirani yake ,Sharifa Nz...

NAIBU WAZIRI MAKAMBA AIPONGEZA PBPA KWA UTENDAJI KAZI MZURI

Picha
Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam  Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba (Mb) ameipongeza Wakala ya Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) kwa utendaji kazi mzuri katika kuhakikisha nchi inakuwa na akiba ya mafuta ya kutosha. Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya PBPA leo jijini Dar es Salaam. "Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya lakini hakikisheni mnatoa elimu kwa Watanzania kuhusu majukumu yenu na kazi zenu" amesema Mhe. Salome. Aidha, ametumia nafasi hiyo kuitaka PBPA kuwawezesha Watanzania wazawa kuingia kwenye biashara ya mafuta na kufanya kazi kwa ushirikiano. "Lazima tupate wawekezaji wa Tanzania, tuwawezeshe waingie kwenye hii biashara " amesisitiza Mhe. Salome. Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala ya Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Bw. Erasto Simon amesema wakala hiyo imefanikiwa kuhakikisha kunakuwa na akiba ya mafuta ya kutosha, uwepo wa takwimu sahihi za kiasi cha mafuta pamoja na kuiwezesha Serikali kupanga ukusanyaji wa mapato. ...

KALEYA MOLLEL ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA SIMANJIRO

Picha
  Na Mwandishi wetu, Simanjiro DIWANI wa Kata ya Msitu wa Tembo, Kaleya Melita Mollel amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, kwa kura zote 24 za Madiwani waliohudhuria kikao. Mwakilishi wa Katibu Tawala wa wilaya ya Simanjiro, Edosi Evaristi Ndikwiki amesema Mollel ambaye ni Diwani wa Kata ya Msitu wa Tembo, amepata kura zote 24 zilizopigwa  Ndikwiki pia amesema, madiwani hao wamemchagua Diwani viti maalum wa Tarafa ya Terrat, Mwanjaa Jacob kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa kura zote 24 za ndiyo. Amesema katika uchaguzi huo uliofanyika  mji mdogo wa Orkesumet ulihusisha madiwani wote wanaotokana na CCM wa kata zote 18 na viti maalumu sita. Ndikwiki amewaasa madiwani hao kutoa ushirikiano kwa wataalam wa halmashauri hiyo kwani wameshaapa kutumikia nafasi zao. "Tuzingatie mahusiano mazuri na watumishi, tuwape ushirikiano na tuwe watatuzi wa migogoro tusiibue migogoro ambayo itaturudisha nyu...

WANANCHI BABATI WAIPA KONGOLE REA

Picha
Mitungi ya gesi 3,255 kusambazwa  na kuuzwa kwa bei ya ruzuku, Mitungi mmoja kuuzwa kwa bei ya ruzuku TZS 17,500. Na Mwandishi Wetu, Babati. Kongole hizo zimetolewa leo, tarehe 04 Disemba, 2025 na wananchi wa kata ya Ayalagaya Wilaya ya Babati mkoani manyara wakati wa usambazaji na uuzaji wa mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku katani hapo. Uuzaji wa majiko hayo umeongozwa na  diwani wa kata ya Ayalagaya Mheshimiwa Sabil John , mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Babati, mtendaji kata ya Ayalagaya , Afisa kutoka REA na mwakilishi wa kampuni Manjis Logistics Limited.  "Kinachofanyika leo ni kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia  katika kutunza mazingira na afya za wananchi" amesema Mhe. Sabil. Mhe. Sabil amesema, Lengo la mradi huu unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ni kuendeleza juhudi za utunzaji wa mazingira na Afya za wananchi kwa kuhakikisha wananchi wanapata elimu  na hamasa ya ...

TCAA YAWEZESHA MAFANIKIO YA REKODI YA DUNIA NDANI YA HIFADHI YA TARANGIRE.

Picha
Na Lubango Mleka, Tarangire. MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeratibu na kusimamia kwa mafanikio safari ya kihistoria ya puto la hewa moto (hot air balloon) iliyoifanya Tanzania kuorodheshwa rasmi kama nchi ya 123 katika jaribio la rekodi ya dunia la kurusha balloon na rubani akiwa pekee yake, lililoendeshwa na Dkt. Rubani Allie Dunnington. Safari hiyo maalum imefanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ikiwa ni mara ya kwanza kwa safari ya aina hii kufanyika na mtu mmoja ndani ya eneo la hifadhi. Uamuzi huu wa kipekee ulifikiwa na TCAA baada ya kufanya tathmini ya kina ya kiusalama, utaratibu wa kiufundi na uhalali wa operesheni ndani ya eneo hilo nyeti. Kwa mujibu wa TCAA, safari hiyo imefuata kikamilifu kanuni, taratibu na viwango vya usalama vya kitaifa na kimataifa. TCAA imeshirikiana kwa karibu na wadau wa uhifadhi pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha zoezi linafanyika kwa usalama, ufanisi na kulinda uadilifu wa mazingira ya hifadhi. Dkt. Ruba...

RACHEL NJAU AMSHUKURU RAIS SAMIA KUWAPATIA WANAWAKE LESENI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani  MAKAMU Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini wanawake Tanzania (TAWOMA) Rachel Joseph Njau amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kuwapatia wanawak leseni za uchimbaji na ununuzi wa madini bila malipo. Hivi karibuni Waziri wa Madini Anthony Mavunde aliwapatia leseni ya uchimbaji madini na leseni ya ununuzi wa madini wanawake na vijana 423 waliopo katika vikundi 21 wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara. Rachel ambaye pia ni Katibu wa chama cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara (MAREMA) Tawi la Mirerani ametoa shukrani hizo kwenye uchaguzi wa TAWOMA Tawi la Mirerani ambapo Magreth Nelson alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa TAWOMA kwa wanawake wafanyabiashara wa magonga ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite. Ameeleza kwamba kitendo cha Rais Samia Suluhu Hassan kuwasaidia wanawake kwenye mpango huo kinaongeza idadi ya wanawake wanaonufaika na sekta ya madini. "Tunampongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kumtuma Waziri Ant...

MAGE NELSON MWENYEKITI MPYA TAWOMA MIRERANI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani  MFANYABIASHARA maarufu wa kuongeza thamani madini ya Tanzanite wa mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Magreth Nelson amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama cha wanawake wanaojihusisha na shughuli za madini Tanzania (TAWOMA) Tawi la Mirerani. Mage atatumikia kwa muda wa miaka mitano nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa wanawake wafanyabiashara wa magonga ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite mji mdogo wa Mirerani. Katika uchaguzi huo uliofanyika chini ya Makamu Mwenyekiti wa TAWOMA, Rachel Joseph Njau na Katibu Mkuu wa TAWOMA, Salma Ernest Kundi na kusimamiwa na Mwenyekiti wa MAREMA Tawi la Komolo Swalehe Abdalah na mjumbe wa MAREMA Tawi la Mirerani Jafar Matimbwa na kushuhudiwa na Afisa maendeleo ya jamii mamlaka ya mji mdogo wa Mirerani Floriana Mcharo. Mwenyekiti wa MAREMA Tawi la Komolo, Swalehe Abdalah akitangaza matokeo hayo amesema Magreth Nelson ambaye hakuwa na mpinzani alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura ...

WAZIRI MAVUNDE AMPONGEZA RMO KASEZA

Picha
Na Mwandishi wetu, Mirerani  WAZIRI wa Madini Mhe Anthony Peter Mavunde, amempongeza Afisa madini mkazi (RMO) wa mkoa wa kimadini wa Mirerani, George Kaseza kwa namna anavyotekeleza wajibu wake ipasavyo, bila kulalamikiwa au kubagua wachimbaji. Waziri Mavunde ameeleza hayo wakati akizungumza na wadau wa madini ya Tanzanite mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, alipofanya ziara ya kutembelea machimbo ya madini ya Tomarini ya kijani eneo la Lemshuku na madini ya Tanzanite mji mdogo wa Mirerani. Amesema RMO Kaseza ni kiongozi mzoefu katika suala zima la eneo tengefu la Mirerani ndiyo sababu akateuliwa kuwa kiongozi wa hapo ambaye wadau wa madini pia wanamkubali kupitia utendaji kazi wake. "RMO Kaseza umekuwa mara nyingi ukiandika maandiko mengi ya eneo tengefu la Mirerani ndiyo sababu tukakuleta hapa sasa yake maandiko yako yafanye kuwa uhalisia ili yaonekane kwa vitendo," amesema Waziri Mavunde. Amewaasa wadau wa madini wa eneo hilo kumpa ushirikiano wa kutos...

URA – SACCOS YAPATA HATI SAFI MIAKA TISA MFULULIZO.

Picha
  Na. Lubango Mleka, Arusha.  KAMISHINA wa fedha na lojistiki (CP) Liberat Sabas amekipongeza Chama cha ushirika cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi (URA SACCOS LTD) kwa kuendelea kupata hati safi kwa miaka tisa (9) mfululizo kutoka kwa mkaguzi wa nje, jambo ambalo limewezesha  kuwa chama bora kitaifa kwa miaka mitano mfululizo na kuwa  chama kinachoongoza kwa mtaji mkubwa, mali na idadi kubwa ya wanachama. Kamishna Sabas yameyasema hayo leo Novemba 28, 2025 wakati akimwakilisha mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Camillius Wambura kufungua mkutano wa 17 wa chama hicho unaofanyika jijini Arusha.   “kupata hati hizo safi kwa mfululizo, zinaakisi uwazi na uadilifu wa uendeshaji makini wa chama chetu” alisema CP Sabas. Matokeo ya ufanisi huo kwa mwaka 2025 yametokana na uongozi bora, nidhamu ya kifedha na moyo wa umoja na  kujituma  kwa watendaji wa chama hicho. CP Sabas aliongeza kuwa uongozi bora na nidhamu ya kifedha imewezesha chama hicho kuwa na ak...