Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei 30, 2026

WAZIRI MAVUNDE ATOA WITO WAMILIKI WOTE WA LESENI ZA UCHIMBAJI WA MADINI KINYWE KUANZA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI MARA MOJA.

Picha
   Lengo ni kuifanya Tanzania kuwa kinara wa uzalishaji wa madini kinywe ifikapo Mwaka 2030, Serikali yasaini mkataba wa ubia na  Kampuni za Grafica na Eminent. Aitaka Timu ya majadiliano ya serikali kuanza mchakato wa majadiliano na Wamiliki wa Leseni 27, Amshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha sekta ya madini, Ruangwa kuwa sehemu ya mnyororo wa thamani na teknolojia ya madini kinywe duniani. Na Mwandishi Wetu, Ruangwa, Lindi.  WAZIRI wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb), ameielekeza Timu ya Majadiliano ya Serikali kwenye Sekta ya Madini (GNT) kuwaita na kufanya nao majadiliano wamiliki wote wa leseni za uchimbaji madini kinywe nchini Tanzania kujadiliana kuhusu ubia wa serikali katika Kampuni hizo na kuwataka kuanza utekelezaji wa uchimbaji kwa mujibu wa masharti ya leseni na Sheria ya Madini Sura ya 123. Ameyasema hayo leo tarehe 30 Mei, 2026 Wilayani Ruangwa aliposhiriki zoezi la utiaji saini na Kampuni za Grafica Resources na Eminent Min...

CHAMA CHA BIBLIA TANZANIA CHA SAMBAZA MAANDIKO ZAIDI YA LAKI TANO MWAKA 2025.

Picha
  Na Wellu Mtaki, Dodoma.  MWENYEKITI wa Bodi ya Chama cha Biblia Tanzania, Askofu Dkt. Mark Malwa Malekana amesema kuwa katika mwaka 2025 chama hicho kimefanikiwa kusambaza jumla ya maandiko 538,544, ikilinganishwa na maandiko 512,650 yaliyosambazwa mwaka 2024.Amesema maandiko hayo yamesambazwa kupitia mifumo na lugha mbalimbali ili kuwafikia Watanzania wengi zaidi. Askofu Malekana ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa Mkutano Mkuu wa 40 wa Chama cha Biblia Tanzania. Ameeleza kuwa chama hicho kimeendelea kupata mafanikio makubwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kueneza Neno la Mungu nchini. Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na ujenzi wa jengo la kitega uchumi la Bible Plaza, maandalizi ya Kamusi ya Biblia, Itifaki ya Biblia pamoja na uchapishaji wa kitabu cha historia ya Chama cha Biblia Tanzania. Pia chama hicho kimefanikiwa kuzindua Biblia za lugha za Kikagulu na Kihehe kwa lengo la kuwafikia waumini wanaotumia lugha hizo za asili. Kwa upande wake, Katibu Mku...