Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 25, 2025

KIWANGO CHA UFAULU MKOANI SINGIDA KUONGEZWA NA MIRADI YA SEQUIP.

Picha
Na Mwandishi Wetu.  WANANCHI wametakiwa kushirikiana na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kulimda miundombinu ya shule iliyojengwa ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi mkoani Singida. Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Halima Dendego wakati akizungumzia tathmini na hali ya elimu leo tarehe 25 Julai 2025 ambapo amesema kuwa uongozi wa mkoa huo umejipanga kuimarisha sekta ya elimu kufuatia maboresho makubwa yanayofanywa ikiwemo ujenzi wa shule mpya. Rc Dendego amesema kuwa jumla ya shule 30 za kata zimejengwa kupitia Mradi wa kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari nchini (SEQUIP) sambamba na ujenzi wa shule mpya 1 ya wasichana ya Solya iliyopo wilayani Manyoni na Ujenzi wa shule 2 mpya za Amali ya Kitukutu iliyojengwa wilayani Iramba pamoja na Unyambwa iliyojengwa katika Manispaa ya Singida. Ameongeza kuwa baada ya ujenzi wa shule hizo mkoa wa Singida umeongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne kutoka asilimia 87 mwa...