Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari 15, 2026

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA WIZARA YA VIWANDA KWA KUENDELEZA KONGANI NA KUSIMAMIA MIRADI YA KIMKAKATI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma. MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mhe. Deodatus Mwanyika, ameipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara kwa hatua inazoendelea kuchukua katika kuanzisha na kuendeleza kongani za viwanda kupitia taasisi zake, hatua inayochochea fursa za ajira na ukuaji wa uchumi nchini. Akizungumza katika kikao cha kwanza cha Kamati hiyo cha kupokea taarifa ya wizara kuhusu muundo, majukumu, sera na sheria kilichofanyika Januari 15, 2026 Bungeni jijini Dodoma, Mhe. Mwanyika,amesema  usimamizi madhubuti wa Wizara katika miradi ya kimkakati na miradi kielelezo kuwa kinaonyesha dhamira ya dhati ya serikali kubadili sura ya sekta ya viwanda.   “Miradi hiyo inapaswa kutekelezwa mapema iwezekanavyo kwa kuwa ina mchango muhimu katika kuongeza ajira, kukuza pato la taifa na kuimarisha uchumi wa viwanda kwa ujumla.”amesema Mhe.Mwanyika. Aidha, ameisisitiza Wizara kuendelea kuboresha sera na sheria ili ziendane na Dira ya Taifa ya Maend...

SERIKALI YASISITIZA MAADILI YA KAZI KWA WATUMISHI WA SERIKALI ZA MITAA

Picha
Na Hamida Ramadhan, Dodoma. WATUMISHI wa Serikali za Mitaa wametakiwa kuzingatia maadili ya kazi na utumishi wa Umma ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima inayosababisha kushambuliana au kurushiana maneno kati yao na Viongozi wakuu wa Serikali au Wanasiasa. Wito huo umetolewa Leo Januari 15,2026 na Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Deus Sangu, alipokuwa akizungumza jijini Dodoma katika Kikao cha 31 cha Baraza la Taifa la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU). Amesema kuwa ili kuondokana na migogoro hiyo, kila mtumishi wa Umma anapaswa kuzingatia maadili ya kazi kwa kuepuka vitendo vya uongo, uzembe, pamoja na ubadhirifu wa fedha na mali za umma. Sangu ameeleza kuwa mikutano ya vyama vya wafanyakazi ni haki ya kikatiba na serikali imekuwa ikishirikiana na vyama hivyo katika kutatua migogoro, ikiwemo kuwatetea watumishi pale wanapotendewa kinyume cha maadili, kama vile kupewa lugha isiyo ya staha au kupewa miradi na kufany...

TANZANIA YASISITIZA UONGEZAJI THAMANI MADINI BARANI AFRIKA

Picha
Tanzania yajipanga kuwa kitovu cha  uongezaji thamani madini Afrika, yashauri kuhusu ushirikiano wa kikanda na kisekta. Na Mwandishi Wetu, Riyadh, Saudi Arabia. TANZANIA imetambua shughuli za uongezaji thamani madini kama nguzo muhimu ya kuleta maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii lengo kubwa ikiwa ni kuondokana na uuzaji na usafirishaji wa madini ghafi kwa nchi zinazozalisha madini mbalimbali Barani Afrika. Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Steven Kiruswa, wakati akizungumza kwenye Kongamano la Kimataifa la Madini lijukanalo kama Future Minerals Forum 2026 lililowakutanisha mawaziri, viongozi mashuhuri na wadau wa sekta ya madini kutoka zaidi ya nchi 100 ndani na nje ya Bara la Afrika.  Dkt. Kiruswa amesema kuwa, rasilimali madini ni moja ya utajiri mkubwa uliopo Barani Afrika hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuweka mkazo katika shughuli za uongezaji thamani madini ndani ya nchi za Afrika ambapo kama kila nchi itazingatia hilo itakuwa moja ya ufunguo wa ...

TASAC YAFANYA UKAGUZI CHUO KIPYA CHA MAFUNZO YA UBAHARIA

Picha
  Na Lubango Mleka, Dar Es Salaam. SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kupitia Mkurugenzi Mkuu ambae pia ni Msajili wa Mabaharia Bw. Mohamed Salum amefanya ukaguzi wa miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika Chuo cha Mafunzo ya Awali ya Ubaharia Cha Dar es Salaam - Dar es Salaam Maritime Training Academy (DMTA) kilichopo mtaa wa Nkurumah jijini Dar Es salaam. Aidha, chuo hicho kimeomba kupewa ithibati ya kufundisha kozi za awali za ubaharia (Basic Safety Training). Tasnia ya ubaharia nchini imepata msukumo mpya kwa sekta binafsi kuanzisha vyuo kwa ajili ya kuongeza ujuzi wa awali katika masuala ya usafiri majini.  Bw. Salum amesema kuwa, Tanzania kuna kundi kubwa la vijana ambao wakitumia fursa ya kujiunga na DMTA itasaidia kujenga safari mpya ya maisha yao.   “Tanzania tuna bahari na maziwa ambayo tukiyatumia vema yatachangia kuongeza ajira kwa vijana na kupunguza ukosefu wa ajira. Hongereni sana uongozi wa DMTA kwa kuanzisha chuo hiki, aidh...

SERIKALI YAAINISHA MKAKATI WA KUWAENDELEZA WACHIMBAJI WADOGO

Picha
  Kipaumbele kikubwa ni leseni za uchimbaji kwa wachimbaji wadogo, Waziri Mavunde aelezea mkakati wa kuwawezesha kimtaji, Kamati ya Bunge yaipongeza BoT kwa ununuzi wa tani 16.4 za dhahabu, Kamati yasisitiza kuongezwa kwa eneo la utafiti madini kutoka asilimia 16 ya sasa. Na Lubango Mleka, DODOMA. SERIKALI imeainisha mkakati mahsusi wa kuwaendeleza wachimbaji wadogo wa madini nchini, kwa kuweka kipaumbele katika utoaji wa leseni, upatikanaji wa mitaji, teknolojia, masoko ya uhakika pamoja na maeneo yenye taarifa za utafiti. Hayo yameelezwa na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, wakati wa kikao cha kwanza cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kilichofanyika leo Januari 15, 2025 katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma. Waziri Mavunde amesema kuwa shughuli zote za utafutaji, uchimbaji, uongezaji thamani na biashara ya madini zinatekelezwa kwa mujibu wa Sera ya Madini ya mwaka 2009 na Sheria ya Madini, Sura ya 123, kwa lengo la kuhakikisha wachimbaji wadogo...

IDRAS ITAONGEZA WIGO WA KODI NA KUSIMAMIA USAWA – CG MWENDA

Picha
Na Lubango Mleka, Dar Es Salaam. KAMISHINA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda amesema Mfumo Jumuishi wa Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani (IDRAS) unaotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni utaongeza wigo wa Kodi na kusimamia usawa katika ulipaji wa kodi. Hayo yamebainishwa na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda alipokuwa akifungua mafunzo ya IDRAS kwa washauri wa kodi na wahasibu jijini Dar es Salaam, Januari 15, 2026 ambayo yatafanyika kwa siku tatu na kuendelea kwa makundi mengine kwa muda wiki mbili. Kamishna Mkuu Mwenda amesema mfumo wa IDRAS unakwenda kufanya maboresho makubwa kwa mifumo ya kodi za ndani iliyopo na unatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika ukusanyaji wa mapato kwa kuweka usawa katika makadirio ya kodi. Amesema kupitia IDRAS wataweza kuwabaini na kuwabana wanaokwepa kodi kwa njia mbalimbali na kuongeza wigo wa kodi kwa kusajili walipakodi wapya huku wakiwezesha biashara za walipakodi na kuzilinda. “Kuwezesha biashara za Walipakodi ni ...

AFISA MTENDAJI MKUU WA GST AANZA KAZI

Picha
Makabiziano ya Ofisi yafanyika,Watumishi wa GST kufanya kazi kwa ushirikiano. Na Hamida Ramadhan, Dodoma. AFISA Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Mhandisi Ally Samaje amewataka watumishi wa GST kufanya kazi kwa ushirikiano ili kukuza Sekta ya Madini hapa nchini kwani Taasisi hiyo ndio moyo wa Sekta hiyo. Mhandisi Samaje ametoa wito huo leo Januari 14,2026 jijini Dodoma katika hafla ya makabidhiano ya ofisi pamoja na kikao alichofanya na watumishi wa GST ambapo amesisitiza watumishi kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuipeleka mbele Sekta ya Madini. “Tufanye kazi kwa ushirikiano kama timu moja ili kuleta mageuzi katika sekta hii ya madini kwani taasisi hii ndio roho ya Sekta ya Madini” Amesema Mhandisi Samaje. Aidha, Mhandisi Samaje amesema Taasisi hiyo ina kazi kubwa ya kufanya tafiti mbalimbali ambazo zitawawezesha wachimbaji wa madini wakubwa na wadogo kufanya shughuli zao kwa ufanisi na kwa uhakika. Sambamba na hayo, Mhandisi Samaje amesisitiza ...