Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 13, 2026

REA YAFANYA ZIARA YA UHAMASISHAJI MIRADI YA NISHATI VIJIJINI MKOANI IRINGA.

Picha
  Wananchi wapewa elimu matumizi  bora ya nishati safi, Wananchi wapewa elimu ya  UMETA (READY BOARD), REA yahamasisha wananchi kujiunga na huduma ya umeme. Na Mwandishi Wetu, Iringa.  WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuhamasisha matumizi sahihi na endelevu ya umeme kwa Watanzania ikiwa ni pamoja na matumizi ya vifaa vya kisasa vya umeme hususan majiko ya umeme ambayo yanatumia kiasi kidogo cha umeme, salama kwa afya za watumiaji na kwa gharama nafuu. Hayo yamebainishwa na Wataalam wa REA waliofika mkoani Iringa wilaya ya Kilolo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kutumia fursa ya miradi ya REA inayotekelezwa mkoani humo. Akizungumza katika mkutano na wananchi, Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka REA, Abdulrazack Mkomi amesema kuwa, majiko ya umeme yanalinda afya za watumiaji na ni nafuu kulinganisha na matumizi mengine ya nishati ya mkaa na kuni. Ameongeza kuwa, ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, REA itaendelea kusambaza kwa wingi majiko ya gesi...