Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari 5, 2026

WITO WA KUCHUKUA HATI KWA WATANZANIA

Picha
 

KIFO CHA MUNDE TAMBWE CHAUMIZA WENGI

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora. ALIYEKUWA Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi kwa miaka 15, Munde Tambwe amezikwa jana katika makaburi ya Shehe Yahaya, Kata ya Ng’ambo Mjini Tabora na kuhitimisha safari yake hapa duniani. Msiba huo umevuta hisia za watu wengi wakiwemo vijana, akinamama, wana CCM, jamii, wabunge na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, kutokana na ushirikiano wake mzuri, ukarimu na kujitoa zaidi kwa jamii enzi za uhai wake. Akiongea kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye msiba huo, Makamu wa Rais Dkt Emanuel Nchimbi ameeleza kuwa marehemu alikuwa rafiki wa kila mtu. Ameongeza kuwa alikuwa mtu mwema kwa jamii, wanaCCM, wabunge na viongozi wenzake na katika nafasi zote azizowahi kutumikia alitanguliza maslahi ya nchi na chama chake, hakuwa na makuu. ‘Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa pole nyingi kwa wanafamilia, jamii, wabunge na wanaCCM wote kwa kuondokewa na mtu muhimu na Kada mwaminifu kwa ch...

WAANDISHI WA HABARI 140 KUJENGEWA UWEZO

Picha
  Na Mwandishi wetu, Arusha. WAANDISHI wa habari 140 wa Tanzania watajengewa uwezo wa kuandika habari za mazingira kupitia kanda mbalimbali nchini. Mkurugenzi wa shirika la waandishi wa habari la kusaidia jamii za asili (MAIPAC) Mussa Juma ameeleza kwamba waandishi hao watajengewa uwezo kupitia mtandao wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC) kwa uwezeshaji wa shirika la umoja wa mataifa UNESCO. Mussa amesema awali wameanza kutoa mafunzo hayo jijini Arusha kwa waandishi wa habari wa mikoa ya kanda ya Kaskazini na kanda ya kati. Amesema waandishi wa habari wa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Manyara, Singida na Dodoma wamepatiwa mafunzo hayo  "Waandishi 140 watajengewa uwezo kwani baada ya kanda ya kaskazini, watafuata waandishi wa kanda ya ziwa, pwani na Zanzibar," amesema Mussa. Amesema waandishi hao watajengewa uwezo wa kuandika habari mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi, athari za mazingira katika migodi na uchafuzi wa mazingira kwenye bahari," amesema Muss...