Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba 22, 2025

YANGA YAICHAPA AS FAR 1–0, YAENDELEA KUWIKA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Picha
  TIMU ya Yanga ambao ni Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wameibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya AS FAR Rabat katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika uliopigwa leo, Novemba 22, 2025, katika Dimba la New Amaan Complex, Zanzibar. Yanga SC walipata bao pekee la mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji wao Prince Dube dakika ya 58, akimalizia kwa ustadi pasi ya kutengeneza nafasi iliyotolewa na Mudathir Yahya. Kwa ushindi huo, Yanga SC wamefanikiwa kuvuna pointi tatu muhimu wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani, na hivyo kujiweka kwenye mazingira mazuri katika harakati zao za kusaka nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo barani Afrika, na kuweka hisroria ya kuwa timu ya kwanza  kupata ushindi.

WAFUGAJI WA JAMII YA KIMASAI HANDENI WAMETAKIWA KUEPUKA MIGOGORO NA KUSHIRIKIANA NA POLISI

Picha
  Na Mwandidhi Wetu, Tanga. WAFUGAJI kutoka vijiji vya Msomela na Kwamantuku, Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga, wametakiwa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kudhibiti matukio ya uhalifu na kudumisha amani katika jamii zao. Wito huo umetolewa leo tarehe 22 Novemba 2025 na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Tanga, ACP Wambura, alipokutana na wawakilishi hao katika kikao cha majadiliano. ACP Wambura amewaasa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi, kutoa taarifa za viashiria vya uhalifu na kuchochea amani katika maeneo yao. Aidha, Wafugaji hao wametoa pongezi kwa juhudi za Polisi Mkoa wa Tanga, na kuahidi kuendeleza mahusiano mema na wakulima, kuepuka migogoro, na kuwa mabalozi wa amani kwa kutoa taarifa za uchochezi au vurugu mara wanapozibaini.

HAMZA ALLY MNGIA AJITOSA UENYEKITI KITETO

Picha
  Na Mwandishi wetu, Kiteto  DIWANI wa Kata ya Dosidosi Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, Hamza Ally Mngia amejitosa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Mngia ambaye ni mara yake ya kwanza kushinda nafasi ya udiwani akizungumza wakati akirejesha fomu ya kugombea amesema yeye bado ni kijana anayeamini uwezo, bidii na ufanisi wa kutumikia nafasi hiyo ya Mwenyekiti pindi akichaguliwa. "Wakati huu Mwenyekiti wa CCM na Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ameonesha wazi kutuamini vijana na kutupa nafasi kubwa mbalimbali za kimaanuzi nchini na hiyo ndiyo sababu iliyonipa nguvu ya kuiomba nafasi hii ya Mwenyekiti wa  Halmashauri ya Wilaya ya kiteto," amesema. Amesema kwa sasa ni kusubiri mchakato na utaratibu wa vikao vya chama na hana hofu na CCM kwani anayo imani kubwa ukilinganisha na sifa zake za kiuongozi alizonazo. "Nikifanikiwa kuteuliwa nikianza kampeni nitaeleza sababu zangu kwanini nim...

WAKUU WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA WASHIRIKI SHEREHE ZA KUTUNUKIWA KAMISHENI KWA MAAFISA WANAFUNZI WA JWTZ.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Arusha. WAKUU wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiwa ni miongoni mwa viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe za kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika sherehe zilizofanyika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli mkoani Arusha tarehe 22 Novemba, 2025 ambapo Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametunuku Kamisheni.

IGP CAMILLUS WAMBURA- TUSIKUBALI KUGAWANYWA KWA SABABU YOYOTE

Picha
Na Mwandishi Wetu, Moshi. MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amewataka Watanzania kutokubali kugawanyika kwa sababu yoyote ile, iwe ya kidini, kisiasa au rasilimali na badala yake waendeleze upendo na amani ya taifa. IGP Wambura aliyasema hayo Novemba 21, 2025 wakati akifunga rasmi Mafunzo ya Awali ya Askari Polisi Kozi Namba 1/2024/2025 katika Shule ya Polisi Tanzania - Moshi, Kilimanjaro. IGP Wambura amesema amani ya nchi ni jambo la muhimu hivyo kila mmoja anawajibu wa kuendeleza amani na usalama wa nchi ambayo imedumu kwa muda mrefu tangu tumepata uhuru. Pia, amewataka watanzania kuendeleza ushirikiano, umoja na mshikamano na Jeshi la Polisi kwa maslahi ya taifa letu. Aidha, IGP Wambura amewataka askari wahitimu kwenda kutekeleza kwa vitendo yale waliyojifunza kwa kuhakikisha kuwa wanaimarisha usalama wa raia na mali zao kwa kudhibiti vitendo vya kihalifu. Vilevile, amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi M...

HASSAN GHAZALY AKABIDHI MATOKEO YA MKUTANO WA VIJANA KWA MEYA JOHANNESBURG.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Johannesburg. HASSAN Ghazaly Mwanachama wa Kamati ya Mawasiliano ya Mfuko wa Ukaguzi wa Maridhiano wa Afrika (APRM) na Mwanzilishi wa Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa, amekabidhi matokeo ya Mkutano wa Tano wa Vijana wa Afrika uliofanyika Afrika Kusini kwa Mheshimiwa Dada Morero, Meya wa Jiji la Johannesburg, na Balozi Marie Antoinette, Mwenyekiti wa APRM. Hatua hiyo imefanyika katika hitimisho la Mkutano wa Vijana wa Afrika, uliofanyika katika Bunge la Panafrika, Afrika Kusini, chini ya kaulimbiu: “Vijana katika Utawala: Kutoka Ahadi hadi Ustawi.” Katika muktadha wa shughuli za mkutano huo, vikao vilishuhudia ushiriki mkubwa wa baadhi ya viongozi mashuhuri wa kikanda na kimataifa, wakiwemo: Rais wa Heshima wa Mkutano, Sharif Fortun Zivania Sharombera; Rais wa Bunge la Afrika, Laila Dahi; Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana ya Bunge la Afrika, Ahmed Bening; Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Afrika, Dkt. Sunshine Minenhl Miendi; Mwenyekiti wa Shirika la Taifa la Maendeleo...

SIMBACHAWENE AONGOZA KIKAO KAZI NA VIONGOZI WA POLISI CHINI.

Picha
Na Lubango Mleka, Arusha. WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene, ameongoza kikao kazi na viongozi wa Jeshi la Polisi nchini kilichofanyika jijini Arusha, Novemba 21, 2025 ikiwa ni mara yake ya kwanza kuongoza kikao hicho baada ya uteuzi wake wa kuongoza Wizara hiyo Waziri Simbachawene ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dennis Lazaro Londo, pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Maduhu Kazi.