Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili 27, 2026

WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA) YASHIRIKI TAMASHA LA KILIMO JIJINI MBEYA.

Picha
Wahamasisha Nishati Safi ya Kupikia.  Na Mwandishi Wetu, Iwambi- Mbeya.  WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) unashiriki katika tamasha la kilimo linalofanyika katika  viwanja vya Iwambi jijini Mbeya kuanzia tarehe 25 mpaka 29 Aprili 2026, ambapo zaidi ya watu 100,000 wakiwemo vijana kutoka mikoa mbalimbali ya kanda ya nyanda za juu kusini wanatarajiwa kushiriki. Wakala unatumia jukwaa hilo kuelimisha na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi pamoja na kueleza hali ya upatikanaji wa huduma ya umeme katika maeneo ya vijijini. Kupitia banda lake, REA imeonesha bidhaa mbalimbali za nishati safi ya kupikia, ambapo bidhaa kuu zinazohamasishwa ni pamoja na matumizi ya majiko ya umeme, majiko ya gesi pamoja na majiko banifu. Teknolojia hizo zimebainishwa kuwa suluhisho muhimu katika kupunguza matumizi ya nishati chafu kama kuni na mkaa, kulinda mazingira na kuboresha afya za watumiaji. Akifungua rasmi maonesho hayo, Kaimu mkuu wa wilaya ya Mbeya ambae pia ni Mk...

BUNGE LAPITISHA BIL. 174.9/- KWA WIZARA YA MADINI

Picha
  Yalenga kuchangia trilioni 1.4/- za maduhuli, Makusanyo yafikia Trilioni 1 na Milioni 156, Jumla ya tani 23.8 za dhahabu zakusaywa ndani ya miezi 18, Ni Juhudi za Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan.  Na Hamida Ramadhan, Dodoma.  Bunge la Jamhuru ya Muungano wa Tanzania, limeridhia na kupitisha bajeti ya Wizara ya Madini ya shilingi bilioni 174.9 kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 ili kuiwezesha Wizara ya Madini kufanikisha ukusanyaji wa maduhuli ya shilingi trilioni 1.4. Akiwasilisha Bungeni makadirio ya Mapato na Matumizi leo Aprili 27, 2026, Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amesema fedha hizo zitawezesha kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara pamoja na taasisi zilizo chini yake, huku zikilenga kuendeleza kasi ya ukuaji wa sekta ya madini kwa kufanya tafiti za jiosayansi nchini. Akifafanua mgawanyo wa Bajeti hiyo, Waziri Mavunde amesema kiasi cha  shilingi bilioni 71.5 sawa na asilimia 40.9 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo, wakati shilingi bilioni 103....

KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YASISITIZA UFANISI WA MIRADI YA MAENDELEO YA SEKTA YA MADINI

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeitaka Serikali kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi yote ya sekta ya madini ili kuhakikisha inaleta manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi na kuimarisha mchango wake katika uchumi wa taifa. Akiwasilisha maoni ya Kamati hiyo bungeni Aprili 27, 2026, Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Simon Lusengekile, alisema Serikali inapaswa kuhakikisha miradi ya maendeleo inapatiwa rasilimali za kutosha pamoja na usimamizi madhubuti ili ikamilike kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa. Alibainisha kuwa usimamizi imara wa miradi hiyo utaongeza tija katika sekta ya madini na kuboresha huduma kwa wananchi kupitia miradi ya kimkakati inayolenga kuongeza thamani ya rasilimali za madini. Kamati imeishauri Wizara kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa kuzingatia mipango ya taifa, viwango vya ubora na muda uliopangwa ili kuepuka ucheleweshaji na kupunguza changamoto za utekelezaji. Aidha, imeitaka Serikali kuimarisha usi...

SERIKALI YAWEKA MKAZO SEKTA YA MADINI KUPITIA VIPAUMBELE NANE 2026/2027

Picha
  Na Hamida Ramadhan, DODOMA WIZARA ya Madini imeweka bayana mkakati wa vipaumbele nane kwa mwaka wa fedha 2026/2027, hatua inayolenga kuifanya sekta hiyo kuwa chachu ya ukuaji wa uchumi, kuongeza ajira na kuhakikisha rasilimali zinasimamiwa kwa ufanisi zaidi. Akiwasilisha mpango wa bajeti bungeni, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, alisema serikali imejipanga kuimarisha utafiti wa madini ili kubaini maeneo mapya yenye utajiri na kuongeza upatikanaji wa takwimu sahihi zitakazovutia wawekezaji zaidi. Alieleza kuwa mkazo pia utawekwa kwenye uongezaji thamani wa madini kwa kuyachakata ndani ya nchi, jambo litakaloongeza mapato ya taifa, kufungua ajira mpya na kuinua thamani ya mauzo ya nje. Katika kuhakikisha Watanzania wananufaika zaidi, wizara inalenga kuongeza ushiriki wao katika mnyororo mzima wa thamani wa madini, hususan kwa kuwawezesha wachimbaji wadogo na wa kati kupitia mafunzo na uwezeshaji wa kitaalamu. Aidha, serikali itaendelea kuwaendeleza wachimbaji wadogo kwa kuwapatia...

BAJETI YA WIZARA YA MADINI 2026/2027 YALENGA KUIMARISHA MAPATO NA USIMAMIZI WA RASILIMALI

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma WIZARA ya Madini imewasilisha ombi bungeni la kuidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 174.98 kwa ajili ya mwaka wa fedha 2026/2027, fedha zitakazotumika kutekeleza majukumu mbalimbali ya sekta hiyo. Akiwasilisha makadirio hayo Aprili 27, 2026, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, alieleza kuwa sehemu ya fedha hizo, takribani shilingi bilioni 71.51 sawa na asilimia 40.87, imepangwa kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo. Kwa upande mwingine, kiasi cha shilingi bilioni 103.47, sawa na asilimia 59.13 ya bajeti yote, kimetengwa kwa matumizi ya kawaida ya wizara pamoja na taasisi zilizo chini yake. Ndani ya fungu hilo, shilingi bilioni 27.36 zitatumika kulipa mishahara ya watumishi, huku shilingi bilioni 76.11 zikigharamia shughuli nyingine za kiutendaji. Waziri Mavunde alisisitiza kuwa utekelezaji wa bajeti hiyo utachangia kuimarika kwa ukusanyaji wa mapato ya serikali, yakilenga kufikia shilingi trilioni 1.4, sambamba na kuboresha usimamizi na uendelezaji wa ...