Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 30, 2025

INEC YAKUTANA NA WAWAKILISHI WA VYAMA VYA SIASA KUPITIA NA KUFANYA MABADIRIKO MADOGO KWENYE MIKUTANO YA HADHARA YA RAIS NA MAKAMU RAIS.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  MKURUGENZI wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Ndugu. Kailima Ramadhani leo tarehe 30 Agosti, 2025 ameongoza kikao cha wawakilishi wa vyama vya siasa kupitia na kufanya mabadiliko madogo kwenye ratiba ya mikutano ya hadhara ya kampeni za wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais. Mikutano hiyo iliyoanza tarehe 28 Agosti, 2025 inaendelea hadi tarehe 28 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Bara na tarehe 27 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Zanzibar. Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara utafanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.

DK.MWINYI:CCM ITAFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU KWA SERA ZENYE TIJA KWA WANANCHI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambaye pia ni Mgombea Mteule wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na kuahidi kuwa CCM itafanya kampeni za kistaarabu zitakazozingatia Utamaduni, Silka na Desturi za Wazanzibari. Dkt. Mwinyi amechukua fomu hiyo katika Afisi za Tume ya Uchaguzi leo, tarehe 30 Agosti 2025, asubuhi, na hatimaye msafara wake ukaelekea Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui kupitia Barabara ya Miembeni, Kariakoo, Rahaleo na Michenzani, akisindikizwa na mamia ya wanachama wa chama hicho waliokuwa wamejipanga pembezoni mwa barabara. Aidha, Dkt. Mwinyi amezuru Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume, na kisha kuzungumza na Wazee wa Chama Cha Mapinduzi afisini hapo. Akizungumza na mamia ya wanachama wa CCM katika Uwanja wa Mao Tse Tung, Mgombea Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesisitiza kuwa...