Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 27, 2025

SHULE 6 MPYA ZAJENGWA NA MRADI WA SEQUIP IRAMBA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Iramba, Singida.  SERIKALI kupitia mradi wa Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) imetumia Bilioni 6.361 kujenga Shule mpya sita za Sekondari, Shule sita zimefanyiwa ujenzi wa upanuzi wa miundombinu ya kidato cha 5 na 6, Ujenzi wa vyoo na nyumba za walimu katika Wilaya ya Iramba Mkoani Singida. Akitoa taarifa ya miradi ya elimu iliyojengwa katika wilaya ya Iramba, Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe. Suleiman Mwenda amesema kuwa ujenzi wa shule hizo utaimarisha sekta ya elimu ikiwemo kuongeza ufaulu wa wanafunzi. Amezitaja shule hizo zilizojengwa wilayani hapo kuwa ni pamoja na ujenzi wa Shule ya Sekondari -MALUGA uliogharimu shilingi milioni 470, ujenzi wa shule ya Sekondari NDULUNGU uliogharimu shilingi milioni 470, ujenzi wa shule ya Sekondari -Mtoa darajani uliogharimu shilingi milioni 544.225. Miradi mingine mipya ni pamoja na ujenzi wa shule ya sekondari -Makunda uliogharimu shilingi milioni 544.225, ujenzi wa shule ya Sekondari-KIZEGA uliogharimu shilin...