Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba 14, 2025

KATIBU MKUU AMWAGA PONGEZI KWA UWT TABORA

Picha
Na Allan Kitwe, Tabora. JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoani Tabora imepongezwa kwa kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwao katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani. Pongezi hizo zimetolewa jana na Katibu Mkuu wa UWT Taifa Suzane Kunambi alipokuwa akiongea na mamia ya Viongozi na wanachama wa Jumuiya hiyo kutoka Wilaya zote 7 za Mkoa huo na vikundi vya wanawake wajasiriamali. Ameeleza kuwa umoja na mshikamano unaoendelea kuoneshwa na akinamama wa UWT Mkoani hapa na wanaCCM wote ni ishara tosha kuwa wagombea wote wa CCM watapata ushindi wa kishindo. ‘Wanawake wa Tabora hongereni, kazi yenu ni njema sana, naamini Oktoba 29 mwaka huu, mtajitokeza kwa wingi zaidi na kumpigia kura za kishindo mgombea Urais kupitia CCM, wabunge na madiwani, CCM Oyeee’, amesema. Kunambi amesisitiza kuwa ni wajibu wa wana UWT kushiriki kikamilifu katika kampeni zinazoendelea sasa hapa nchini na kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kumsemea Dk Samia Su...

JULIUS NYERERE: BABA WA TAIFA LA TANZANIA

Picha
Na Dkt. Gazaly, Egypt. MWALIMU Julius Kambarage Nyerere amezaliwa tarehe Aprili 13, 1922 na alifariki dunia tarehe 14 Oktoba, 1999. Leo ni kumbukumbu ya miaka 26 tangu kifo chake. Alisoma katika Chuo cha Makerere mjini Kampala, Uganda, kisha akaendelea na masomo katika Chuo Kikuu cha Edinburgh, Scotland, akiwa Mtanganyika wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza, na wa pili pekee kupata shahada ya chuo kikuu nje ya Afrika. Mnamo mwaka 1952 alirudi Tanganyika, akaoa, na kufanya kazi kama mwalimu. Mnamo mwaka 1954, alisaidia kuanzisha Chama cha Tanganyika African National Union (TANU), chama kikuu cha kisiasa katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika kutoka kwa utawala wa Uingereza. Nyerere alihubiri mapambano yasiyo ya kutumia nguvu ili kufanikisha lengo hilo. Katika uchaguzi wa Baraza la Kutunga Sheria wa mwaka 1958–1959, Nyerere alichaguliwa kuwa mbunge. Baadaye, aliongoza TANU kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1960 na akawa Waziri Mkuu. Mazungumzo yake na viongozi...