LISHE BORA SHULENI YATAJWA KUWA MSINGI WA MAFANIKIO YA ELIMU
Na Jasmine Shamwepu, Dodoma KAMISHINA wa Elimu Tanzania, Dk Lyabwene Mtahabwa, amesema mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji hauwezi kufanikiwa bila kuwepo kwa huduma bora za chakula na lishe shuleni. Amesisitiza kuwa wadhibiti ubora katika halmashauri zote wanapaswa kuhakikisha chakula kinachotolewa kwa wanafunzi kinazingatia viwango vya ubora ili kuepusha madhara ya kiafya ikiwemo viriba tumbo. Dk Mtahabwa alitoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mradi wa CRISP unaotekelezwa na SwissAid kwa miaka mitatu katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Dar es Salaam. Amesema maboresho ya elimu hayawezi kuleta matokeo chanya kama hayatazingatia lishe ya wanafunzi, akibainisha kuwa serikali imeweka sera na miongozo kuhakikisha shule zinatoa huduma ya chakula. “Mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji hatuwezi kufanikiwa bila kuwa na huduma bora za chakula na lishe,” amesema Dk Mtahabwa. Ameeleza kuwa serikali imechukua hatua mbalimbali kuimarisha lishe shuleni, ikiwemo waraka wa mwaka 2...