Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari 25, 2026

MALALAMIKO YA VIWANJA MBADALA YAPATIWA UFUMBUZI DODOMA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  SERIKALI kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeyapatia ufumbuzi malalamiko ya muda mrefu ya viwanja mbadala kwa wananchi wa jiji la Dodoma. Suluhisho hilo linafuatia malalamiko ya takriban wananchi 4000 wa jiji la Dodoma wanaodai viwanja na halmashauri ya jiji la Dodoma kuwapa ahadi bila kutekeleza mpaka sasa. Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 25 Februari 2026 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo wakati akizungumza na wananchi wenye migogoro ya ardhi katika eneo la Mahomanyika lilopo kata ya Nzuguni jijini Dodoma. Dkt Akwilapo amesema, eneo la Mahomanyika ni eneo la serikali hivyo lipangwe na kupimwa kwa ajili ya utatuzi wa migogoro ya meneo mbalimbali ya jiji la Dodoma pamoja na matumizi ya serikali. "Eneo hili lenye mgogoro hapa Mahomanyika ni eneo la serikali hivyo lipangwe na kupimwa kwa ajili ya utatuzi wa migogoro na siyo ya hapa tu na mingine ya jiji la Dodoma na matumizi ya serikali...

TAKUKURU MKOA WA MWANZA IMEFANIKIWA KUDHIBITI KIASI CHA TZS MILIONI 85.5

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Mwanza.  TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza imefanikiwa kudhibiti kiasi cha Sh milioni 85.5 kupitia uchambuzi wa mfumo wa malipo ya fedha za kujikimu kwa walimu wa shule za sekondari katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza. Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, Abnery Mganga, amesema kuwa katika utekelezaji wa majukumu ya kuzuia rushwa, taasisi hiyo ilifanikiwa kudhibiti kiasi hicho cha Sh milioni 85.5 na kuhakikisha kinalipwa kwa walimu waajiriwa wapya wa shule za sekondari waliokuwa na madai katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza. Aidha, Mganga amesema mafanikio hayo yametokana na uchambuzi wa mfumo uliofanywa na taasisi hiyo pamoja na halmashauri kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa katika kikao kazi kati ya TAKUKURU na wadau wa halmashauri. Hatua hiyo imewawezesha walimu 77 waliokuwa na madai kulipwa stahiki zao.

CCM: MAKAMPUNI YASIYOLIPA WAKULIMA YAPIGWE ‘STOP’

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeitaka Bodi ya Tumbaku (TTB) nchini kuchukua hatua mara moja dhidi ya Makampuni yote yanayonunua zao la tumbaku na kushindwa kulipa wakulima kwa wakati, na kushauri wapigwe stop. Ushauri huo umetolewa jana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Komredi Saidi Nkumba alipokuwa akitoa salamu za chama katika Mkutano Mkuu wa 33 wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Tumbaku (WETCU) Mkoani Tabora. Amesema kuwa haingiii akilini kuona mkulima akihangaika kuandaa shamba lake mwaka mzima tena kwa gharama kubwa ili kuhakikisha anapata tumbaku nzuri inayokidhi viwango vya soko la ndani na nje lakini anapouza halipwi kwa wakati. ‘Chama Cha Mapinduzi hakifurahishwi na hali hii, Wanunuzi wote wanaokuja kununua mazao ya wakulima wanatambulika kisheria na wanapewa leseni, kama hawafanyi kile kinachotakiwa kuna haja gani ya kuwabembeleza’, ameeleza. Komredi Nkumba ameitaka Bodi ya Tumbaku kusimamia ipasavyo zao hilo ili mkulima anufaike na jasho...