MMOJA AFARIKI, WAWILI WAJERUHIWA WAKIBISHANIA SIMBA NA YANGA
Na Mwandishi Wetu, Mwanza. MTU mmoja amefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kutokea ugomvi uliozuka kutokana na ushabiki wa mpira kati ya mashabiki wa timu za Simba na Yanga Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza. Kwa mujibu taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa amesema tayari wameanzisha msako wa kumtafuta kijana mmoja (jina limehifadhiwa) kwa tuhuma za kumuua Abel Mganga Mazuri (25) mkazi wa Nyamahengo, na kuwajeruhi watu wawili kufuatia ugomvi uliotokana na ushabiki wa mpira. Taarifa hiyo imesema tukio hilo limetokea Machi 24, 2026 majira ya saa 5:30 usiku katika kitongoji cha Nyamahengo, kijiji na kata ya Sumve, wilayani Kwimba, mkoani Mwanza. "Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limeanza msako wa kumtafuta kijana mmoja (jina limehifadhiwa kwa sasa) kwa tuhuma za mauaji ya Abel Mganga Mazuri, miaka25, mkazi wa Nyamahengo aliyeuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kifuani kisha kuwajeruhi watu wawili kwa kutumia kitu c...