Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba 15, 2025

CHATANDA ASHIRIKI KIKAO CHA BARAZA MAALUM LA UWT WILAYA YA KINONDONI

Picha
  Na Hamida Ramadhani, Dar es Salaam. MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) ambaye pia ni Mratibu wa Kampeni za CCM Jijini DSM, Leo tarehe 15 Oktoba, 2025, akutana na wajumbe wa Baraza la UWT Wilaya ya Kinondoni kwenye Ofisi za CCM Wilayani humo, katika kuandaa Hamasa na kupeana mikakati zaidi ya kumuombea Kura za kishindo Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wagombea Ubunge na Udiwani wa CCM, pamoja na kufanya maandalizi ya Mikutano ya Kampeni ya Dkt. Samia ndani ya Jiji la DSM kwa kunadi ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025/2030 kwa Wananchi ili wajitoke kwa Wingi siku ya kupiga kura Oktoba 29, 2025 na kuwachagua Wagombea wote wa CCM.

WATUHUMIWA WANNE WAKAMATWA KWA KUENDESHA TELEVISHENI YA MTANDAONI BILA LESENI

Picha
 

TFF YAUFUNGIA UWANJA WA SOKOINE MBEYA

Picha

RAIS DKT. SAMIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

Picha
Chanzo cha picha,IKULU. RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametuma salamu za rambi rambi baada ya kifo cha mwanasiasa wa upinzani nchini Kenya, bwana Raila Odinga. Kupitia ukurasa wake wa Instgram Samia amesema, "imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Raila Amolo Odinga. Tumempoteza kiongozi mahiri, Mwanamajumui wa Afrika, mpenda amani na mtafuta suluhu, ambaye ushawishi na upendo wake haukuwa tu ndani ya Kenya, bali Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Msiba huu si wa Kenya pekee, bali wetu sote." Tunaungana kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awajalie subra, faraja na imani katika kipindi hiki, na ailaze roho ya mpendwa wetu, Mheshimiwa Raila Amolo Odinga, mahali pema peponi.

POLISI PWANI WACHANGIA DAMU HOSPITALI YA RUFAA TUMBI.

Picha
LEO tarehe 15, Oktoba 2025 Kikosi cha Afya Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na hospitali ya Rufaa ya Tumbi Mkoani humo wameendesha zoezi la uchangiaji damu kwa askari likiwa na lengo la kusaidia wahitaji katika hospitali hiyo.