Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba 1, 2025

MICHEZO

Picha
RATIBA ya Michuano ya Kagame Cup 2025.   

DKT. LADISLAUS CHANG’A ASHIRIKI KATIKA MKUTANO WA 6 WA MAWAZIRI NA MAMLAKA ZA MAZINGIRA WA ASIA NA PASIFIKI

Picha
Nadi, Fiji.  KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang’a, kwa mwaliko wa Programu ya Umoja wa Mataifa uratibu wa Mazingira (UNEP) ameshiriki kikamilifu katika Mkutano wa 6 wa Mawaziri na Mamlaka za Mazingira wa Asia na Pasifiki (6th AP Forum) uliofanyika kuanzia tarehe 26–29 Agosti 2025 Jijini Nadi, Fiji. Mkutano huo uliandaliwa kwa pamoja na Serikali ya Fiji na UNEP ukiwa na kaulimbiu “Kutafuta Suluhisho Endelevu katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi Duniani”. Sambamba na mkutano huo, Dkt. Chang’a alikuwa na vikao mbalimbali na waheshimiwa na taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kikao na Mhe. Rupa B. K., Waziri wa Serikali ya Nepal, Wizara ya Misitu na Mazingira, ambapo alimpatia taarifa kuhusu mpango kazi wa IPCC unaotekelezwa hadi mwaka 2029.  Mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano wa kikan...

REA YAENDELEA KUTEKELEZA KWA VITENDO MKAKATI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Picha
 *Majiko banifu 4,836 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoa wa Njombe.  Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 8,850 tu.  📌 *Kila walaya kupata majiko 1,209*  Na Mwandishi Wetu, Njombe.  KATIBU Tawala wa Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omari amekutana na Timu ya Wataalam kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) leo Septemba 1, 2025 na kupata taarifa ya mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku ambao unatarajia kuanzia mapema mwezi wa 9, 2025. Akiwasilisha taarifa ya mradi kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Mhandisi wa miradi Kutoka wakala wa Nishati Vijijini, Raya Majallah, amesema, Wakati Taifa likiwa kwenye mkakati wa kuhakikisha Watanzania wanatumia nishati safi na salama ya kupikia, Wakala wa Nishati Vijijini umekuja na mpango wa usambazaji na uuzaji wa  majiko banifu 200,000 kwa bei ya ruzuku yanayotumia kuni na mkaa mchache sana na yenye ufanisi mkubwa katika matumizi yake. Mradi huu umekuja kwa lengo la kuimarisha na kubor...

WANANCHI WAHIMIZWA KUACHA MATUMIZI YA MKAA NA KUNI, WATAKIWA KUTUMIA MAJIKO YA NISHATI SAFI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  ILI kupunguza madhara ya kiafya na kimazingira yanayosababishwa na matumizi ya kuni na mkaa, wananchi wametakiwa kuachana na nishati hizo na kuhamia kwenye matumizi ya majiko yanayotumia umeme na sola kupitia kampeni ya kitaifa ya Pika Smart. Kampeni hii imefika mkoa wa tano kwa Dodoma huku lengo likiwa ni kuelimisha jamii kuhusu faida za kutumia nishati safi kwa gharama nafuu ambayo inalenga kupunguza utegemezi wa nishati zisizo salama na zisizo endelevu. Akizungumza wakati wa kampeni hiyo Septemba Mosi jijini Dodoma, Rightness Felix Balozi wa Pika Smart, amesema kuwa matumizi ya kuni na mkaa yana gharama kubwa kwa familia na yana madhara kwa afya na mazingira.  “Kwa kutumia majiko ya umeme, mtu anaweza kupika kwa gharama ndogo sana. Kwa mfano, unaweza kutumia shilingi 1,000 tu na ukapika mlo wako bila moshi wala madhara ya kiafya tuna vifaa salama kabisa, tofauti na mitazamo iliyokuwepo awali kuwa majiko ya umeme yanapiga shoti,” amesema Felix. Am...

MICHEZO

Picha
NAIBU katibu Mkuu wa Wizara  ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Felister Mdemu amewaaga wanamichezo wa wizara hiyo watakaoshiriki katika michezo ya Shirikisho la Michezo kwa wizara na Idara za serikali leo Septemba 1, 2025 kuelekea Jijini Mwanza. Felister ametoa rai kwa washiriki hao kuwa makini na kujali afya zao pindi wanapokuwa katika mashidano hayo ili waweze kurejea salama na kuendelea na majukumu yao.

TAARIFA KWA UMMA

Picha