SERIKALI, WADAU WAWEKA MIKAKATI KUKABILI VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI
Na WAF, Dodoma. Serikali kupitia Wizara ya Afya, Idara ya Afya ya Uzazi wa Mama na Mtoto, kwa kushirikiana na Shirika la Thamini Uhai wamekutana pamoja na kuweka mikakati utekelezaji wa Mradi wa Ushirikiano wa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, Dkt. Ahmad Makuwani wakati wa kikao hicho kilichofanyika leo Januari 21, 2026 katika Ofisi za Wizara ya Afya Mtumba jijini Dodoma. "Serikali imeweka nia ya dhati ya kuhakikisha inaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi kwa kushirikisha wadau mbalimbali ili kufanikisha utekelezaji wa mradi huo," amesema Dkt. Makuwani. Ameongeza kuwa ni muhimu kwa Wizara ya Afya kupitia Idara ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto ikuweka mikakati bora ya namna ya kutekeleza mradi huo ikiwa ni pamoja na kuangalia maeneo yanayopaswa kupewa kipaumbele katika mradi huo ikiwemo ujenzi wa majengo ya uangalizi maalum wa mtoto wenye changamoto mba...