DAWA NA VIFAA TIBA VYA MIL 822.8 VYAKAMATWA TABORA
Na Allan Kitwe, Tabora . MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Magharibi imefanya oparesheni maalumu na kufanikiwa kukamata dawa zenye thamani ya sh mil 822.8 zilizokuwa zinauzwa kinyume na utaratibu. Hayo yamebainishwa jana na Meneja wa TMDA Kanda ya Magharibi, Christopher Migoha alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, ambapo alieleza kuwa jumla ya kilo 2,300 zenye thamani ya shilingi mil 822.8 zimekamatwa na kuteketezwa. Amefafanua kuwa dawa na vifaa tiba hivyo vimekamatwa katika oparesheni maalumu iliyofanyika katika hospitali, vituo vya afya, zahanati na maduka ya dawa baridi za binadamu na mifugo katika Wilaya zote. Migoha ameeleza kuwa dawa hizo haziruhusiwi kuuzwa katika maduka ya watu binafsi na ni kinyume cha sheria na kanuni ya 63 ya mwaka 2005 ya dawa zilizozuiliwa kuuzwa hadharani hususani katika maduka ya watu binafsi. Ameongeza kuwa katika operesheni hiyo walikagua jumla ya maduka 408 ya dawa, Hospital 16, vituo vya afya 17, zahanati 17, famas...