Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 16, 2025

MHANDISI SANGA AONGEZA MWEZI MMOJA KLINIKI YA ARDHI KIVULE KUONGEZA KASI YA UTOAJI HATI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.  Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga ameongeza mwezi mmoja kwa watumishi wanaotoa huduma za ardhi kwenye Kliniki ya Ardhi inayofanyika Kata ya Kivule Ilala Dar e salaam kuanzia Agosti 18, 2025 ili kupunguza mzingo mkubwa kwa wananchi ambao hawana hati. Mhandisi Sanga ametoa maekelezo hayo Agosti 16, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Kivule ambao wanaendelea kupata huduma kwenye Kliniki hiyo.  “Tunatamani zoezi hili limalize changamoto zenu zote, kwa sababu tukimaliza changamoto zenu hapa hamtakuja ofisini, nawaagiza wasaidizi wangu, zoezi hili liendelee kwa muda wa mwezi mzima baada ya tarehe 18 Agosti 2025 ambayo ilipangwa ili kumaliza changamoto zenu za ardhi katika maeneo yenu” amesema Mhandisi Sanga. Ili kuleta tija katika zoezi hilo, Mhandisi Sanga ameelekeza watumishi 10 waongezwe katika kliniki hiyo ambao watatoka maeneo mbalimbali nchini ili kuongeza kasi y...