MISRI YAADHIMISHA KUMBUKUBU YA UHURU WA SINAI.
Na Hassan Ali Ghazaly, Misiri. KILA mwaka 25 Aprili, Misri huadhimisha kumbukumbu ya uhuru wa Sinai, baada ya uondoaji wa majeshi ya Israel kutoka eneo hilo mwaka 1982. Siku hii huenzi tukio muhimu katika historia ya kisasa ya taifa la Misri. Pia inaakisi mafanikio ya juhudi za kisiasa katika kurejesha ardhi. Uhuru wa Sinai ulitokana na mazungumzo na makubaliano ya kimataifa, pamoja na mchango wa jeshi la Misri katika Vita vya Oktoba 1973. Pia, Serikali inaendelea kuadhimisha kumbukumbu hii kila mwaka kupitia shughuli rasmi na kuelimisha vizazi vipya. #NasserForum #nasseryouthmovement #NLF #hassanghazaly #NasserNet #habarikamilitv #uzalendokwanza