Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 7, 2025

MUUGUZI BANDIA AKAMATWA BAADA YA KUHUDUMIA WAGONJWA ZAIDI YA 4,000 FLORIDA.

Picha
MWANAMKE mmoja amekamatwa nchini Marekani kwa tuhuma za kujifanya muuguzi aliyesajiliwa. Uchunguzi wa polisi ulianzishwa baada ya wakuu wa hospitali kukatisha kandarasi ya Autumn Bardisa kutokana na wasiwasi kuhusu sifa zake za kikazi. Wachunguzi waligundua kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwa ametoa huduma za matibabu kwa wagonjwa 4,486 kati ya Juni 2024 na Januari 2025. "Hii ni moja ya kesi za kutatanisha zaidi za udanganyifu wa kimatibabu ambazo tumewahi kuchunguza," Mkuu wa Kaunti ya Flagler Rick Staly alisema. Bardisa aliajiriwa na AdventHealth Palm Coast Parkway huko Palm Coast kuanzia Julai 2023 hadi Januari 2025. Anadaiwa kuwasilisha hati za uwongo na kutoa nambari ya leseni ya muuguzi aliye na jina moja la kwanza ambaye aliajiriwa na AdventHealth katika hospitali tofauti. Ofisi ya Kaunti ilisema alielezea tofauti hiyo kwa kudai kwamba alikuwa ameolewa hivi majuzi na amebadilisha jina lake la ukoo. Aliombwa kutoa leseni yake ya ndoa lakini hakufanya hivy...

TRUMP KUKUTANA NA PUTIN

Picha
RAIS Donald Trump wa Marekani amedokeza kuwa atakutana na na rais wa Urusi Vladimir Putin ana kwa ana hivi karibuni ili kujadili usitishwaji wa vita vinavyoendelea nchini Ukraine. Trump amesema mkutano wake na Putin ni matokeo ya mazungumzo yenye tija kubwa yaliyofanyika mjini Moscow kati ya mjumbe wake maalum Steve Witkoff na Rais Putin. Urusi tayari imethibitisha kuhusu mkutano huo huku Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky nae akitoa wito wa kukutana ana kwa ana na Putin ili kuzungumza namna ya kuvimaliza vita hivyo vilivyodumu kwa zaidi ya miaka mitatu.  #USA #Trump #Russia 

DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AKUTANA NA WANA MICHEZO ZANZIBAR.

Picha
KUMBUKUMBU KATIKA MICHEZO..  ZANZIBAR :- Kabla ya kuanza ujenzi wa viwanja vya michezo na maeneo rasmi ya mazoezi, Mgombea Urais wa CCM Zanzibar mwaka 2020, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, alikutana na wanamichezo katika maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba kwa lengo la kusikiliza changamoto sugu walizokuwa wakikabiliana nazo na kufahamu mazingira halisi ya michezo Zanzibar. Kipindi cha kampeni za Urais za mwaka 2020, Dkt. Hussein Ali Mwinyi hakutilia mkazo hotuba ndefu majukwaani, bali aliamua kushuka mitaani, kukutana na wanamichezo, makocha na mashabiki. Aliahidi si tu kuboresha mazingira ya michezo, bali pia kuwezesha ndoto za wanamichezo wa Zanzibar kutimia. Picha hii ni ushahidi wa Uongozi Unaoacha Alama. Kwa bashasha na ukaribu, Dkt. Hussein Ali Mwinyi alikutana na wadau mbalimbali wa michezo, akashiriki nao mchezo wa mpira wa mikono, na hatimaye kuwaahidi kuwa siku za matumaini kwa maendeleo ya sekta ya michezo Zanzibar zinakuja.