Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba 10, 2025

SENDIGA AZINDUA MRADI WA USAMBAZAJI NA UUZAJI WA MAJIKO BANIFU KWA BEI YA RUZUKU MANYARA.

Picha
 *Majiko banifu 7,914 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku, Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 11,200.  Na Mwandishi Wetu, Manyara. MKUU wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga, leo Novemba 10, 2025 amezindua rasmi mradi wa uuzaji na usambazaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku mkoani Manyara. Uzinduzi huu ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa upatikanaji na uhamasisha wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia. Aidha,uzinduzi huu umefanyika katika Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Manyara iliyopo wilaya ya Babati, ambapo jumla ya majiko banifu  7,914 yatauzwa na kusambazwa kwa bei ya ruzuku ya kiasi cha  TZS 11,200 ambayo ni sawa na aslimia 80 ya ruzuku ya TZS 56,000 ambayo ni bei ya awali ya jiko. Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mheshimiwa Sendiga amesema mpango huo umelenga kuhakikisha wananchi wote, hususani wa kipato cha chini, wanapata fursa ya kutumia nishati safi na salama ya kupikia kwa gharama nafuu. Aidha, amewaagiza Wakuu wa Wilaya...

SERENGETI BOYS YAWASILI ADDIS ABABA

Picha
  Timu ya Taifa U17 (Serengeti Boys) imewasili Addis Ababa, Ethiopia kwenye mashindano ya kufuzu AFCON 2026 Kanda ya CECAFA. @serengetiboystz

MWENYEKITI WA KAMATI YA USALAMA BARABARANI MKOA WA TABORA AKABIDHI GARI KWA JESHI LA POLISI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Tabora. Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Tabora, Bw. Hamud Nasor,  leo Novemba 10, 2025 amekabidhi  gari aina ya Toyota Probox kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard Abwao kwa ajili ya matumizi ya kikosi cha usalama barabarani.