Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 21, 2025

BODI YA USHAURI TARURA YAIPA HEKO SERIKALI UJENZI DARAJA LA MOHORO

Picha
Na Mwandishi Wetu, Rufiji.  MWENYEKITI wa Bodi ya Ushauri ya Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Florian Kabaka ameishukuru Serikali kwa kuwezesha Wakala huo kutekeleza ujenzi wa daraja la Mohoro lenye urefu wa Mita 100 wilayani Rufiji. Mhandisi Kabaka ameyasema hayo wakati wa ziara ya kutembelea ujenzi wa daraja hilo pamoja na ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa Km. 4 zinazojengwa katika mji wa Ikwiriri wilayani humo. “Niipongeze serikali kwa uwezeshaji huu kwa TARURA, kwakweli uwepo wake hata wananchi wanaishukuru kwa kufungua miundombinu kila mahali, nitoe heko kwa serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwa TARURA pia nitoe heko kwa menejimenti ya TARURA kwa usimamizi”. Aidha, amewataka wananchi wa eneo hilo kulitunza daraja hilo pamoja na vifaa vyote vinavyozunguka, pia kutochezea tuta la daraja hilo kwani linaenda kuleta uhakika wa mawasiliano yao kwa mwaka mzima hususan kipindi cha mvua. “Daraja hili linaenda kuwaondolea shida iliyodumu kwa miaka min...