Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei 4, 2026

RC TABORA APEWA TUZO MAALUMU

Picha
Na Allan Kitwe, Tabora CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Tabora kimetoa tuzo maalumu kwa Mkuu wa Mkoa huo Paul Matiko Chacha kama ishara ya kutambua na kuthamini mchango wake katika suala zima la kusimamia maendeleo ya Mkoa huo. Tuzo hiyo imetolewa juzi kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ngazi ya  Mkoa baada ya Wajumbe wa mkutano huo kuridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na Kiongozi huyo hivyo kupendekeza apewa tuzo katika kikao hicho. Awali, akielezea tuzo hiyo, Katibu wa CCM Mkoa Wilson Nkambaku amesema kuwa pendekezo la kutoa tuzo hiyo lilitolewa na Wajumbe katika Kikao kilichopita, hivyo chama kimelifanyia kazi na sasa wapo tayari kumkabidhi. Ameongeza kuwa chama pia kitatoa tuzo kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mheshimiwa Said Juma Nkumba kama ishara ya kutambua kazi yake njema ya kuimarisha, kudumisha na kujenga mshikamano thabiti ndani ya chama. Akikabidhi tuzo kwa Mkuu wa Mkoa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Said Juma Nkumba amesema kuwa Chama kimeridhishwa na kazi yake, anatekeleza...

REA YAMTAMBULISHA MTOA HUDUMA WA MAJIKO BANIFU KAGERA.

Picha
Wananchi Kunufaika na Ruzuku ya Asilimia 80. Na Mwandishi Wetu, Bukoba-Kagera WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) umemtambulisha rasmi mtoa huduma, kampuni ya Burn Manufacturing Company Limited, kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahaya Ramadhani Kido, ikiwa ni hatua muhimu katika utekelezaji wa mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku kwa wananchi wa mkoa huo. Utambulisho huo umefanyika katika kikao kilichowakutanisha viongozi wa mkoa pamoja na wataalamu kutoka REA, ambapo ilielezwa kuwa kampuni hiyo itahusika moja kwa moja na usambazaji wa majiko hayo pamoja na kuhakikisha yanawafikia wananchi kwa bei nafuu kupitia utaratibu wa ruzuku uliowekwa na Serikali.  Mradi huo unalenga kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia na kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa, ambavyo vimekuwa na athari kubwa kwa afya za wananchi na mazingira. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahaya Ramadhani Kido, ameipongeza REA kwa kuendelea kuibua na kusimamia...

SERIKALI YATAKA MATUMIZI SAHIHI YA MITANDAO KUJENGA JAMII NA KULINDA KISWAHILI

Picha
  Na Jasmine Shamwepu, Dodoma.  WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, Amezindua ofisi mpya za Jumuiya ya Wanahabari ya Mitandao ya kijamii Tanzania (JUMIKITA),Tawi la Dodoma aidha ameitaka JUMIKITA kutumia mitandao ya kijamii kujenga jamii yenye maadili na kuendelea kulinda utamaduni wa Kitanzania kupitia matumizi sahihi ya Kiswahili. Ameyasema hayo Mei 3, 2026 jijini Dodoma wakati akizindua ofisi za JUMIKITA Tawi la Dodoma katika eneo la Ilazo. Aidha, amebainisha kuwa Kiswahili ni sehemu ya utambulisho wa taifa na Afrika kwa ujumla, huku akibainisha kuwa Tanzania kupitia UNESCO imeendelea kupewa heshima kubwa katika kukuza lugha hiyo duniani. Ameeleza kuwa mwaka huu Tanzania inatarajia kushiriki maadhimisho ya Kiswahili duniani yatakayofanyika mjini Paris, Ufaransa.  Aidha, Makonda amebainisha kuwa mitandao ya kijamii inapaswa kutumika kuelimisha na kujenga jamii badala ya kusambaza maudhui yanayoharibu maadili ya taifa. Amesema kuwa wanamitan...

WAFANYABIASHARA SOKO LA REHEMA NCHIMBI WALALAMIKIA KUKWAMA KUFANYA BIASHARA DODOMA

Picha
Na Hamida Ramadhan, Dodoma.  WAFANYABISHARA zaidi ya 300 wa Soko la Rehema Nchimbi jijini Dodoma, waliohamishwa baada ya eneo hilo kuchukuliwa na Bunge Oktoba mwaka jana, wameuomba uongozi wa Jiji la Dodoma kuondoa zuio la kuendesha biashara katika eneo mbadala la Umoga walilopewa na Waziri Mkuu. Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti katika eneo la Umonga, baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema ni zaidi ya miezi saba sasa hawajafanya biashara yoyote, hali inayochangia ugumu wa maisha yao. Prisca Chibwaye, mmoja wa wafanyabiashara hao, amesema tangu walipoondolewa kwenye eneo lao la awali wamekuwa wakifuatilia kupata eneo mbadala bila mafanikio. “Mwaka jana tuliondolewa kwenye vibanda vyetu vya biashara bila kupewa taarifa wala fidia baada ya Bunge kuchukua eneo lile lakini tunashukuru serikali kupitia mkuu wa mkoa alisimamia tukaletwa katika eneo hili la Umonga lakini jiji hawataki tufanye biashara hapa,” amesema. Ameongeza kuwa Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba ali...