Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba 16, 2025

MIILI YA WATU WANNE YAKUTWA KANDO YA BARABARA MAPINGA PWANI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Pwani. JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani, limethibitisha kutokea kwa vifo vya wanaume 4 ambao miili yao imekutwa pembezoni mwa barabara ya Mapinga kuelekea Kibaha, ikiwa na majeraha usoni na miguuni. Miili hiyo ambayo ilisafirishwa hadi Hospitali ya Rufaa ya Tumbi kwa uchunguzi zaidi na baadaye, wazazi na ndugu waliweza kuitambua miili hiyo ya vijana wanne kuwa ni wakazi wa Dar es Salaam, ambao ni Mikidadi Abbas Mikidadi (21), Hassan Juma Jumanne (21), na Fadhili Patrick Hiyola (19) amba oni deiwaka wa bodaboda Pamoja na dereva bajaji Abdalla Fadhil Nyanga (21) ambao wote walikuwa wanafanya shughuli zao Dar es Salaam. Jeshi la Polisi limesema miili hiyo imekabidhiwa kwa familia kwa taratibu za mazishi baada ya uchunguzi wa kitabibu kukamilika huku uchunguzi wa kina kubaini mazingira na wahusika wa mauaji hayo unaendelea. Jeshi la Polisi mkoani Pwani limetoa wito kwa wananchi kutoa taarifa yoyote inayoweza kusaidia kufichua ukweli wa tukio hilo na kusisitiza kuwa ushiriki...

NIKOSA KISHERIA KUHAMASISHA MTU ASIPIGE KURA

Picha
 

KORTINI KWA KULAWITI MTOTO WA MIAKA 8

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Mwanza. MKAZI wa Luchelele na mfanyabiashara, Seif Msumari Hozza (26), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza leo Oktoba 16, 2025 kwa tuhuma za kulawiti mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8 (jina limehifadhiwa kwa sababu za kisheria). Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mhe. Aman Sumari, Wakili wa Serikali Rose Kimaro ameieleza mahakama kuwa tukio hilo lilitokea kati ya mwezi Agosti na Septemba 2025 katika eneo la Siluvin, Kata ya Luchelele jijini humo, ambapo mshtakiwa anadaiwa kutenda kitendo hicho cha ukatili dhidi ya mtoto huyo. Katika kesi hiyo ya jinai yenye namba 25168/2025, mshtakiwa anakabiliwa na shtaka moja la kulawiti, kinyume na Kifungu cha 154(1)(a)(2) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, marejeo ya mwaka 2023. Hata hivyo, mshtakiwa amekana shtaka hilo. Hakimu Sumari anayesikiliza kesi hiyo ameeleza kuwa kosa hilo linadhaminika kwa masharti, ikiwemo kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho...

KIRUSWA , NASSARY, MILLYA NA SENDEKA WAONGOZA MAMIA KWENYE MAZISHI YA MAMA WA FRANONE

Picha
  Na Mwandishi wetu, Arumeru NAIBU Waziri wa Madini Dkt Stephen Kiruswa, wagombea ubunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassary, wa Simanjiro James Ole Millya na aliyekuwa mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka, wamewaongoza mamia ya wakazi wa mikoa ya Arusha na Manyara, kwenye mazishi ya mama wa mmoja wa wamiliki wa kitalu C katika machimbo ya madini ya Tanzanite Onesmo Mbise yaliyofanyika kijiji cha Kwaugoro Wilayani Arumeru. Mama wa mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzanite ya Franone Mining LTD inayomiliki kitalu C, Onesmo Mbise, marehemu Apaililia Metasheiye Mungure amezaliwa mwaka 1954 na kufariki dunia mwaka 2025 na kuzikwa katika kijiji cha Kwaugoro wilayani Arumeru. Naibu Waziri Dkt Kiruswa, akizungumza kwenye maziko hayo ametoa pole kwa wakazi wa eneo hilo na kuwaombea faraja kwa Mungu kwenye kipindi hiki kigumu cha msiba. Amesema wafanyakazi wa Wizara ya Madini sekta ya madini kwa ujumla wanatoa pole kwa Onesmo Mbise kwa msiba mkubwa wa kufiwa n...

DKT. MPANGO: MAKUMBUSHO YA KISASA YA NGORONGORO KUKUZA UTALII WA KIHISTORIA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Karatu. MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, amezindua rasmi Makumbusho ya Urithi wa Kijiolojia ya Ngorongoro–Lengai, yaliyogharimu zaidi ya Sh. bilioni 35 ambayo yanatarajiwa kuongeza kasi ya ukuaji wa utalii wa kihistoria na kielimu nchini. Makumbusho hayo yapo katika eneo la Ngorongoro–Lengai Geopark, linalotambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kama Geopark pekee Kusini mwa Jangwa la Sahara na ya pili barani Afrika. Akizungumza leo Oktoba 16,2025 katika uzinduzi huo wilayani Karatu, Dkt. Mpango amesema kukamilika kwa makumbusho hayo ni hatua muhimu katika kukuza utalii wa urithi na historia, sambamba na kutangaza vivutio vya asili vya Tanzania kimataifa.  “Geopark hii siyo tu hifadhi ya historia, bali ni chachu ya elimu, tafiti na maendeleo ya jamii zinazozunguka eneo hili,” amesema Dkt. Mpango. Dkt. Mpango ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha shughuli zote za ut...

KAMPENI YA TUWAAMBIE KABLA HAWAJAHARIBIKA YAZINDULIWA UYUI

Picha
Na Lubango Mleka, Uyui. KAMPENI ya “Tuwaambie Kabla Hawajaharibiwa” awamu ya pili imezinduliwa Oktoba 14, 2025 katika ukumbi wa VETA Uyui, ikiambatana na maandamano kutoka stendi ya Isikizya. Uzinduzi huo umeongozwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Uyui, SSP Edward J. Ituja, huku Afisa Tarafa Shaban Said akimwakilisha Mkuu wa Wilaya, Mh. Mohamed Mtulyakwaku kama mgeni rasmi. Washiriki walihusisha wanafunzi wa shule za msingi, sekondari, na chuo cha VETA, viongozi wa dini, wazazi na maafisa wa polisi. Viongozi hao waliwahimiza vijana kuepuka matumizi ya dawa za kulevya, ukatili wa kijinsia na makundi hatarishi, huku wazazi wakisisitizwa kuchukua jukumu la malezi. Mgeni rasmi aliwataka wanafunzi kutumia mitandao kwa uangalifu na kuwa mabalozi wa nidhamu na maadili mema katika jamii.

HABARI PICHA

Picha
MKUU wa Polisi Wilaya ya Mbulu Mkoa wa Manyara Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Kelvin Haule Oktoba 14, 2025 akiwa ameambatana na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai  ASP Mbosela  ameongoza mafunzo maalumu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 kwa askari mgambo wilayani humo ikiwa ni muendelezo wa Jeshi la Polisi kutoa elimu ya uchaguzi kwa askari mgambo ili kuwawezesha kusimamia   haki na kufanya kazi kwa weledi kwenye uchaguzi huyo. Sambamba naye ASP Mbosela ametoa elimu ya Sheria mbalimbali za uchaguzi kwa askari hao ili kuwaongezea uelewa juu ya sheria mbalimbali za uchaguzi kuelekea uchaguzi mkuu 2025

RADA DUNIANI ZINAFUATILIA ZAIDI NDEGE ILIYOBEBA MWILI WA RAILA ODINGA

Picha
Chanzo cha picha, AFP Ndege iliyobeba wajumbe wa Kenya yenye mwili wa Raila Odinga kutoka India imekuwa ikifuatiliwa zaidi duniani kwenye Flightradar24. Mara tu baada ya kupaa saa 6:30 jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi, ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la Kenya KQA202 hadi Mumbai ilikuwa ya pili kwa kufuatiliwa duniani kote kwenye huduma maarufu ya kufuatilia trafiki ya moja kwa moja. Kufikia saa sita usiku, ilikuwa imefuatiliwa zaidi duniani kote, ikiwa na zaidi ya watu 7,000 wakiifuatilia. Ndege ilifika Mumbai mwendo wa saa 1 asubuhi Alhamisi, Saa za Afrika Mashariki (EAT), na kupaa kuelekea Nairobi saa tis ana nusu Alfajiri saa za Afrika Mashariki. Inatarajiwa kutua uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta mwendo wa saa 9:30 asubuhi Saa 7 asubuhi, data ya Flightradar24 ilionyesha kuwa ndege ya kurudi KQA203 ilikuwa ikifuatiliwa na zaidi ya watu 5,000. KQ imesema kuwa ndege hiyo itabadilishwa jina kuwa RAO001, rejeleo la herufi za jina la Odi...

ACT -WAZALENDO ZANZIBAR YAFUNIKA KIBABE KASKAZINI PEMBA.

Picha
  LEO Mgombea wa Urais wa Zanzibar, kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Ndugu @othmanmasoudothman ameendelea na mikutano yake ya Kampeni, akinadi Sera na kuomba ridhaa ya katika Viwanja vya Wingwi Mapofu, Kaskazini Pemba. Oktoba#LindaKura#ZanzibarMamlakaKamili