Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba 12, 2025

ZAIDI YA WANANCHI 1,500 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJIKO BANIFU WILAYANI BABATI

Picha
  Majiko banifu 1,582 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku, Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 11,200. Na Lubango Mleka, Babati. MKUU wa Wilaya ya wa Babati, Mheshimiwa Emmanuela Kaganda, leo Novemba 12, 2025 kwa niaba ya wakazi wa wilaya ya babati amezindua mradi wa uuzaji na usambazaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku.   Uzinduzi huu ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya mkuu wa mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga akiwataka wakuu wa wilaya wote wa mkoa wa manyara kuzindua na kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku katika wilaya zao. Uzinduzi umefanyika katika kata ya Magugu wilayani babati, ambapo jumla ya majiko banifu  1,582 yatauzwa na kusambazwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 11,200 ambayo ni sawa na aslimia 80 ya ruzuku ya TZS 56,000 ambayo ni bei ya awali ya jiko. Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mheshimiwa Kaganda amesema mpango huo umelenga kuhakikisha wananchi wote, hususani wa kipat...

BALOZI PINDI CHANA AKIPA KATIKA KATIKA KIKAO CHA PILI CHA BUNGE LA TANZANIA

Picha
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe,Mhe. Balozi Dkt.Pindi Chana akiapa rasmi kuwa mbunge katika Mkutano wa Kwanza, Kikao cha Pili cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Novemba 12,2025.