Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei 20, 2026

SIKU YA NYUKI DUNIANI’ YAADHIMISHWA KITAIFA TABORA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora.  MAADHIMISHO ya Siku ya Nyuki Duniani yanayoyohusisha utundikaji mizinga, maonesho ya bidhaa na mazao ya nyuki yameanza leo katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Vita Mjini Tabora na kuvuta umati mkubwa wa wananchi. Wakizungumza kwenye maadhimisho hayo wakazi wa Tabora wameeleza kufurahishwa na tukio hilo kwa kuwa linawapa fursa wageni kutembelea Mkoa huo na kuonja utamu wa asali inayozalishwa katika misitu ya Mkoa huo. Daud Elisha, mjasiriamali mkazi wa Kata ya Kanyenye, Halmashauri ya manispaa ya Tabora ameeleza kuwa zao la asali ni miongoni mwa mazao ya kujivunia yanayozalishwa katika Mkoa huo na kuuzwa kwa bei kubwa ndani na nje ya nchi. ‘Haya maadhimisho ni fursa muhimu sana kwa wana Tabora kuuza asali yao na kupanua wigo wa uzalishaji zao hilo katika Wilaya zote za Mkoa huu, hivyo kuwaneemesha zaidi kiuchumi’, amesema. Amina Madereka, mjasiriamali anayejishughulisha na utundikaji mizinga na uuzaji asali katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ame...

TANROADS YAENDELEA KULINDA BARABARA.

Picha
  Na Ahmed Ahmed - Dodoma.  WAKALA wa Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea kulinda miundombinu ya barabara ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kuwa salama kwa watumiaji wakati wote. Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ameyasema hayo Mei 20, 2025 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2026/2027. "Kwa hakika haya ni mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya muda mfupi kwa upande wa miundombinu ya barabara na madaraka," alisema. Ulega amesema barabara zinaendelea kuwa miundombinu muhimu ya usafiri nchini kutokana na kufika katika maeneo mengi ikilinganishwa na miundombinu mingine ya usafiri na usafirishaji. Amesema katika kipindi cha Julai 2025 hadi Aprili 2026, ukarabati wa kawaida ya barabara zenye urefu wa kilomita 16,782.58 umefanyika pamoja na marekebisho maalum ya kilomita 1,101.12.

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2026 AIPONGEZA REA UHAMASISHAJI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Madaba, Ruvuma.  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026 ,Ndugu Wazo Michael Mwang’onda ameipongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa juhudi kubwa inazoendelea kuzifanya katika utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia nchini, akieleza kuwa miradi hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi, salama na rafiki kwa mazingira. Pongezi hizo amezitoa wakati alipotembelea banda la REA katika maonesho yanayoendelea sambamba na Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma, ambapo alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na wakala huo katika kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanapata huduma ya nishati safi ya kupikia kwa gharama nafuu. Akizungumza mara baada ya kutembelea banda hilo, kiongozi huyo amesema REA imeendelea kuwa chachu muhimu katika utekelezaji wa ajenda ya taifa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi pamoja na...