Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 3, 2025

MADALALI WA MINADA WATAKIWA KUJISAJINI KIELEKTRONIKI.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  WIZARA ya Fedha imeandaa Mfumo wa Kielektroniki wa utoaji Leseni za Udalali na Uendeshaji minada ya hadhara unaowezesha uombaji na upatikanaji wa Leseni kwa njia ya kielektroniki kwa kutumia simu za mkononi au kompyuta mpakato ili kuwaondolea wananchi adha na gharama ya kufuata leseni hizo jijini Dodoma. Akizungumza wakati akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Jijini Dodoma, Msimamizi wa Mali za Serikali wizarani hapo, Bw. George Killo, alisema Mfumo huo utamuwezesha mwananchi kufanya usajili popote alipo hivyo kupata leseni yake kwa wakati. ‘‘Mwombaji wa leseni ya udalali anapaswa kujisajili kupitia Tovuti ya Wizara ya Fedha (www.mof.go.tz) na kisha kubonyeza kipengele cha GAMIS na kujisajili, kujaza taarifa zinazohitajika, kujaza fomu za maombi kikamilifu na kuwasilisha kwa Katibu Tawala wa Wilaya husika kwa ajili ya uhakiki na Saini,’’ alieleza Bw. Killo. Alise...

Total Energies CHAN 2024

Picha
FT’ Madagascar 0️⃣ - 0️⃣ Mauritania

RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALI MBALI.

Picha
 

MAONYESHO YA NANE NANE KANDA YA ZIWA MAGHARIBI 2025 YAFUNGULIWA RASMI

Picha
Na Lubango Mleka, Mwanza. MGENI rasmi Mhe. Hashimu Abdallah Komba, Mkuu wa Wilaya ya Geita akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita Ndg. Martin Shigela leo tarehe 03 Agosti 2025, amefungua rasmi maonesho ya Nanenane kanda ya ziwa Magharibi yanayofanyika viwanja vya Nyamhongolo Wilaya ya Ilemela ambapo amesema kila mmoja anao wajibu wa kutembelea maonesho haya ya nane nane kwa ajili ya kujifunza lakini pia kujioatia bidhaa mbalimbali.  “Kama ni mkulima utapata fursa ya kujifunza kilimo cha kisasa na Chenye tija na kama ni mvuvi pia unaweza kujifunza shughuli za uvuvi kwa teknolojia ya kisasa hivyo msiache kutembelea mabanda mbali mbali kujipatia elimu na uzoefu ” Alilisitiza muwakilishi huyo wa mgeni rasmi Mhe Komba.  Akifafanua kauli mbiu ya maonyesho ya Nanenane Mwaka huu “Chagua viongozi bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi 2025” amewataka wananchi kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu na kuchagua viongozi bora watakaowaletea maendeleo.

PPAA YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE, KUTOA ELIMU KWA WAZABUNI NA UMMA.

Picha
 Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  MAMLAKA ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) inashiriki Maonesho ya NaneNane Kitaifa yanaendelea katika Viwanja vya Maonesho vya Nzuguni Jijini Dodoma kutoa elimu kuhusu ununuzi wa Umma kwa wazabuni, hususan elimu kuhusu Moduli ya kupokea na kushughulikia Malalamiko na Rufaa katika mfumo wa NeST.  Akiongea kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa PPAA, James Sando, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma, Nelson Kessy amesema PPAA imejipanga kutoa elimu kwa wadau wa ununuzi wa umma na wananchi kwa ujumla ili kutoa wigo mpana zaidi kwa wazabuni na wadau wa sekta hiyo.  Pamoja na mambo mengine, Kessy amewasihi wadau wa ununuzi na wananchi kwa ujumla kutembelea Banda la PPAA linalopatikana ndani ya Banda la Wizara ya Fedha katika viwanja vya Nzuguni, Dodoma. Maonesho haya kwa mwaka 2025 yamebeba kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025”. Maonesho ya NaneNane Kitaifa yalifunguliwa rasmi t...