Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 12, 2025

ASKARI WANAFUNZI 15 WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI.

Picha
Na Lubango Mleka, Moshi.  ASKARI Wanafunzi 15 wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori la mizigo aina ya Fuso katika eneo la Kwasadala, wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro. Mkuu wa Mkoa huo, Nurdin Babu amesema askari hao walikuwa wakitokea eneo la mazoezi ya medani za kivita la Kilele Pori, lililoko wilayani Siha, wakiwa kwenye gari aina ya Land Cruiser lililogongana uso kwa uso na Fuso. Majeruhi wa ajali hiyo iliyotokea leo Agosti 12, saa sita mchana wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya KCMC na Hospitali ya Wilaya ya Hai. 

TCRA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI SAHII NA SALAMA YA HUDUMA YA MAWASILIANO.

Picha
MENEJA wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ofisi ya Zanzibar, Bi. Esuvatie-Aisa akitoa dondoo muhimu kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano katika kipindi maalumu cha Kituo cha Crown FM Zanzibar tarehe 12 Agosti, 2025 Unguja - Zanzibar.  TCRA inaendelea kutoa elimu kwa umma ikisisitiza matumizi sahihi na salama ya huduma za mawasiliano na kukumbusha wajibu wa watumiaji wa kusambaza taarifa za ukweli na uhakika na kufuta na kutosambaza ujumbe au taarifa zinazochochea upotoshaji, uzushi, chuki na uvunjifu wa amani. #tcratz #elimukwaumma #futadeletekabisa

WACHIMBAJI WADOGO 25 KATIKA MGODI WA NYANDOLWA WAMEFUKIWA NA KIFUSI.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga.  JUMLA ya wachimbaji wadogo 25 katika mgodi mdogo wa Nyandolwa uliopo kijiji cha Mwongozo Halmashauri ya Shinyanga, wamefukiwa na kifusi baada ya mgodi kutitia. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na wachimbaji katika eneo hilo wamefanya juhudi za kuwaokoa wachimbaji hao na tayari wachimbaji wawili wameokolewa. Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro amesema kuwa wachimbaji hao walikuwa katika mashimo matatu tofauti, ikiwemo shimo la duara namba 106 lenye watu 6, 103 lenye watu 11, na duara namba 20 lenye watu 8. Juhudi za uokoaji bado zinaendelea. Tukio la kutitia kwa mgodi huo limetokea Agosti 11, 2025 saa nne asubuhi, wakati shughuli za matengenezo ya maduara hayo zikiendelea. Mtatiro amewasihi wachimbaji kuwa watulivu wakati jitihada za kuokoa uhai wa walioko chini zikiendelea.

VIWANGO VYA KUBADIRISHIA FEDHA ZA KIGENI HAPA NCHINI.

Picha

RAIS MWINYI:SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MASLAHI YA WALIMU.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewahakikishia walimu kuwa Serikali itaendelea kuimarisha maslahi na mazingira ya ufundishaji na kujifunza kwa dhamira ya kuboresha elimu zaidi.  Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 12 Agosti 2025, katika kongamano la kumpongeza lililoandaliwa na Shirikisho la Walimu Zanzibar kufuatia mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu nchini katika kipindi cha uongozi wake. Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein, Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja. Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa, katika kuongeza motisha kwa walimu, Serikali imeboresha maslahi yao kwa kuongeza mishahara, posho za likizo na ufiwa, pamoja na kulipa malimbikizo mengine. Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali  imeajiri walimu wapya 5,265 na kuwapatia mafunzo mbalimbali ili kuongeza ufanisi wao. Ameeleza kuwa kiasi cha shilingi bilioni 1.8 kimetumika katika mwaka wa ...