ASKARI WANAFUNZI 15 WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI.






Na Lubango Mleka, Moshi. 

ASKARI Wanafunzi 15 wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori la mizigo aina ya Fuso katika eneo la Kwasadala, wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa Mkoa huo, Nurdin Babu amesema askari hao walikuwa wakitokea eneo la mazoezi ya medani za kivita la Kilele Pori, lililoko wilayani Siha, wakiwa kwenye gari aina ya Land Cruiser lililogongana uso kwa uso na Fuso.

Majeruhi wa ajali hiyo iliyotokea leo Agosti 12, saa sita mchana wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya KCMC na Hospitali ya Wilaya ya Hai. 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.