Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba 21, 2025

IGP CAMILLUS WAMBURA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA AWALI YA ASKARI POLISI KOZI NO:1/2024/2025 CCP MOSHI.

Picha
Na Lubango Mleka, Moshi. MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, leo Novemba 21,2025 amefunga rasmi Mafunzo ya Awali ya Askari Polisi Kozi No: 1/2024/2025 katika Shule ya Polisi Moshi Kilimanjaro. Akifunga mafunzo hayo IGP Wambura, amewataka askari wahitimu kwenda kutekeleza kwa vitendo yale waliyojifunza kwa kuhakikisha wanaimarisha usalama wa raia na mali zao kwa kudhibiti vitendo vya kihalifu. IGP Wambura, ameendelea kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa ajira ndani ya Jeshi la Polisi pamoja na mambo mengine ikiwemo suala la kuimarisha miundombinu. Jumla ya wahitimu 4826 wakiwemo wapiga buruji wamehitimu mafunzo hayo ya awali yaliyodumu kwa muda wa miezi kumi na mbili na askari hao wahitimu wamejengewa uwezo katika maeneo mbalimbali ya kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika nchini.

DC LULANDALA AMFUTA MACHOZI MJANE SIMANJIRO

Picha
  Na mwandishi wetu, Simanjiro MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mwalimu Fakii Raphael Lulandala amemfuta machozi mjane Sion Mathayo mkazi wa kitongoji cha Mkumbi mji mdogo wa Orkesumet kwa kufanikisha kulipa Sh11 milioni ya deni la nyumba yake iliyowekwa rehani na mume wake  dereva bodaboda Mohamed Ally (Mang'ati) aliyeuawa hivi karibuni. Dereva bodaboda huyo Mohamed Ally (Mang'ati) ambaye aliuza nyumba yake ili kufidia deni alilokuwa anadaiwa, aliuawa kwa kumwagiwa petroli na kuchomwa moto na watu wawili alipokuwa na pikipiki yake Oktoba mwaka 2025 kisha akafariki dunia akipatiwa matibabu. Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Lulandala akizungumza wakati akimkabidhi mjane huyo hati ya nyumba hiyo amesema wadau mbalimbali wamechanga fedha na kulipa deni hilo ili aendelee kuishi na mtoto wake kwenye nyumba hiyo, baada ya mumewe kuuawa. "Mume wake kabla hajafariki alipata masaibu na kuuza rehani nyumba yao kwa Sh11 milioni ili alipe deni analodaiwa kisha akachomwa moto na ...

TUZO ZA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) MSIMU WA 2024/2025

Picha

IGP CAMILLUS WAMBURA KUFUNGA RASM MAFUNZO YA AWALI KOZI NO:1/2024/2025 LEO CHUO CHA POLISI MOSHI.

Picha

KAMPENI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA YAPAMBA MOTO HANANG.

Picha
Majiko 1,583 kuuzwa na kusambazwa kwa bei ya ruzuku, Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya Tsh 11,200. Na Lubango Mleka, Hanang. MKUU wa wilaya ya Hanang Mheshimiwa Almishi Hazali ametoa wito kwa wananchi wa wilaya ya Hanang kujitokezo kwa wingi  kununua majiko banifu ambayo yameanzwa kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku. Wito huo umetolewa leo tarehe 20 Novemba, 2025 na Mheshimiwa Hazali alipofika katika Tarafa ya Katesh Kata ya Nangwa kijiji cha Nangwa kukagua na kufatilia utekelezaji wa mradi ambapo jumla majiko 1,583 yatasambzwa  na kuuzwa kwa bei ya ruzuku wilaya nzima. “Mradi huu unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ni mwendelezo wa  juhudi za serikali  katika kutunza mazingira na kuboresha afya za  wananchi kwa kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kutosha ya umuhimu wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia”alisema Mhe. Hazali. Akizungumza wakati wa uuzaji wa majiko hayo, msimamizi wa mradi kutoka REA, Ndugu Abdulrazack Mkomi ames...