Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei 8, 2026

REA KUIMARISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KUPITIA MAJIKO BANIFU MKOANI MWANZA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Mwanza. WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) umemtambulisha rasmi mtoa huduma, kampuni ya Envotec Services Limited, kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa Said Mtanda, kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku kwa wananchi wa mkoa huo. Utambulisho huo ni sehemu ya juhudi za Serikali kupitia REA za kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini, kwa lengo la kuboresha afya za wananchi, kupunguza matumizi ya nishati zisizo rafiki kwa mazingira pamoja na kuhifadhi mazingira. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mtanda, ameipongeza REA kwa kuendelea kutekeleza na kusimamia miradi mbalimbali ya nishati yenye manufaa kwa wananchi, ikiwemo mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku. Amesema mradi huo ni muhimu kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza kwani utasaidia kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia, kupunguza matumizi makubwa ya kuni na mkaa pamoja na kusaid...

KONGAMANO LA UPANDIKIZAJI VIUNGO VYA BINADAMU KUFANYIKA DODOMA.

Picha
Na Ahmed Ahmed - Dodoma.  KONGAMANO la Kimataifa la Kisayansi la Wataalamu wa Upandikizaji Viungo linatarajiwa kufanyika jijini Dodoma. Akizungumza hivi karibuni jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Prof. Abel Makubi amesema madaktari bingwa wa upandikizaji wa viungo vya binadamu zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali duniani wanatarajiwa kushiriki. "Madaktari hao watatoka katika nchi za Italia, Uingereza, Japani, Afrika Kusini, na Tanzania, lengo la kongamano hilo litakalofanyika kwenye ukumbi wa Domiya ni kuiimarisha Tanzania kwenye ramani ya upandikizaji viungo," alisema. Upandikizaji viungo ni moja ya mafanikio makubwa ya tiba ya kisasa ndani ya taaluma ya Upasuaji wa Kisasa na Immunolojia.  Hata hivyo, utekelezaji wake hutofautiana sana kati ya nchi kutokana na sheria, tamaduni, miundombinu ya afya, na uelewa wa jamii.