KONGAMANO LA UPANDIKIZAJI VIUNGO VYA BINADAMU KUFANYIKA DODOMA.
Na Ahmed Ahmed - Dodoma.
KONGAMANO la Kimataifa la Kisayansi la Wataalamu wa Upandikizaji Viungo linatarajiwa kufanyika jijini Dodoma.
Akizungumza hivi karibuni jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Prof. Abel Makubi amesema madaktari bingwa wa upandikizaji wa viungo vya binadamu zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali duniani wanatarajiwa kushiriki.
"Madaktari hao watatoka katika nchi za Italia, Uingereza, Japani, Afrika Kusini, na Tanzania, lengo la kongamano hilo litakalofanyika kwenye ukumbi wa Domiya ni kuiimarisha Tanzania kwenye ramani ya upandikizaji viungo," alisema.
Upandikizaji viungo ni moja ya mafanikio makubwa ya tiba ya kisasa ndani ya taaluma ya Upasuaji wa Kisasa na Immunolojia.
Hata hivyo, utekelezaji wake hutofautiana sana kati ya nchi kutokana na sheria, tamaduni, miundombinu ya afya, na uelewa wa jamii.

Maoni