Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba 6, 2025

WANANCHI WA SHIGELA-BUSEGA WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA FISI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Simiyu. Wananchi wa Kijiji cha Shigela, Wilaya ya Busega mkoani Simiyu wametakiwa kuwa waangalifu na kuchukua tahadhari dhidi ya fisi wanaoripotiwa kuvamia makazi ya watu na kuleta hofu katika jamii. Rai hiyo imetolewa  Oktoba 6, 2025 na Afisa Uhifadhi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Lusato Masinde, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo ambapo timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, TAWA na Maafisa Wanyamapori wa Halmashauri inaendelea kutoa elimu ya uhifadhi mkoani humo ili kupunguza madhara yatokanayo na wanyamapori wakali na waharibifu.  “Tuchukue tahadhari kubwa, hatuko salama kwa sababu katika mazingira yetu hawa wanyamapori wapo na kuna vichaka na mapango mengi,” amesisitiza  Masinde. Ameongeza kuwa watoto ndio waathirika wakubwa wa mashambulizi ya fisi, hivyo wananchi wanapaswa kuwa makini na kuhakikisha wanawalinda ipasavyo, hasa wakati wa jioni na usiku. Kwa upande wake, Afisa Maliasi...

MAFUNZO YA MADAKTARI BINGWA YASAIDIA KUOKOA MAISHA MKOANI DODOMA

Picha
 Na WAF-Dodoma MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amesema kambi ya madaktari bingwa kupitia mafunzo kwa wataalam imewezesha kuokoa maisha ya wengi kutokana na uwezo waliojengewa wa kushughulikia wagonjwa wa dharura na majeruhi wa ajali kwa haraka na kwa ufanisi. Mhe. Senyamule ameyasema hayo leo Oktoba 06, 2025 wakati akiwapokea wataalam wa afya wabobezi 42 wakiwepo Madaktari Bingwa na Wauguzi Bobezi ambao watafanya kazi ya kutoa huduma kwenye halmashauri za wilaya saba (7) za mkoa wa Dodoma. “Ubunifu huu uliofanywa na Serikali wakuwajengea uwezo wataalam wetu ngazi ya msingi, lakini pia kuanzishwa kwa majengo ya dharura sisi tumeona matunda yake, kwani hivi karibuni tulipata ajali katika wilaya yetu ya Chemba kutokana na utaalam ambao mliwawezesha watu wetu, kuwahudumia  majeruhi wote na kuwafikisha ngazi ya RRH wakiwa salama,” amesema  Mhe. Senyamule. Kwa upande wake Mwakilishi wa Wizara ya Afya Bi. Subira Said, amesema shabaha ya zoezi hilo ni kusogeza hu...

WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA KUONGEZA UWAJIBIKAJI KATIKA KUTOA HUDUMA BORA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma. KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi ametoa wito kwa Watumishi wa Umma kuongeza uwajibikaji na kutoa huduma bora kwa Watumishi wa Umma kutoka katika taasisi mbalimbali, Wadau na Wananchi wanaohitaji kuhudumiwa kwenye masuala ya kiutumishi kwenye Wiki ya Huduma kwa Mteja iliyoanza tarehe 06 hadi 10 oktoba, 2025 yenye kaulimbiu isemayo 2025 Dhamira Inayowezekana.  Bw. Mkomi ametoa wito huo wakati akizungumza na watumishi wa ofisi yake katika eneo maalum la mafunzo kwa watumishi hao yanayofanyika kila siku ya Jumatatu Mtumba Jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi watumishi wa ofisi hiyo. “Hii ni Wiki ya Huduma kwa Mteja, ninatoa wito kwa kila mtumishi kuwajibika katika eneo lake la kazi hasa mnapotoa huduma kwa Watumishi wa Umma wenzenu, Wadau na Wananchi hakikisheni mnatimiza malengo ya Serikali katika kutoa huduma bora kwa kila Mtanzania.” amesema Bw. Mkomi. Kwa upande wake Mwezeshaji ...

DKT. MWINYI: AMANI NI HOJA YA KWANZA YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Konde - Kaskazini Pemba. MGOMBEA wa nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa amani ya nchi ndiyo hoja ya kwanza na ya msingi ya Chama Cha Mapinduzi, akisisitiza kuwa maendeleo hayawezi kupatikana bila kudumisha amani na umoja wa wananchi. Akihutubia mamia ya wanachama wa CCM na wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Michezo wa Msuka, Jimbo la Konde, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dkt. Mwinyi alisema wananchi wana wajibu wa kuilinda amani iliyopo kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo. Mkutano huo ulihudhuriwa na makundi mbalimbali ya wananchi wakiwemo wavuvi, wajasiriamali, mama lishe, waendesha bodaboda, akinamama na wajane. Aidha, Dkt. Mwinyi amesema kuwa CCM inajivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kuimarisha umoja na maridhiano ya Wazanzibari, jambo lililowezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo Unguja na ...

POLISI WAANZA UCHUNGUZI KUHUSU KUTEKWA KWA POLEPOLE, WAKISISITIZA KUMUHITAJI KWA DCI

Picha
Na Hamida Ramadhani.Dodoma. JESHI la Polisi nchini Tanzania, kupitia kwa Msemaji wake DCP David Misime, limesisitiza kuwa bado linaendelea kumsubiri Ndugu Humphrey Polepole ili aripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusu tuhuma mbalimbali alizozitoa kupitia mitandao yake ya kijamii. Ikumbukwe kuwa mnamo Jumatatu, Septemba 15, 2025, Jeshi la Polisi lilitangaza kuwa limefungua jalada la uchunguzi na linaendelea kuchunguza tuhuma hizo ambazo kada huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amekuwa akizitoa.  "Tuhuma ambazo ametoa na anaendelea kuzitoa, kulingana na jinsi alivyozielezea, zinaashiria uwepo wa makosa ya jinai kwa mujibu wa sheria, makosa haya yanahitaji ushahidi wa kuzithibitisha zitakapowasilishwa mahakamani. Tuhuma hizo amekuwa akizitoa kupitia mitandao ya kijamii. Baada ya kufungua jalada na kuanza uchunguzi, Jeshi la Polisi, mbali na kukusanya ushahidi, limekuwa likifanya jitihada za kumpata ili aweze kutoa maele...

FDH SPORTS PROMOTION YAZINDUZI MASHINDANO YA MPIRA KUHAMASISHA NISHATI SAFI

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma. TAASISI ya FDH Sports Promotion imezindua rasmi mashindano ya mpira wa miguu yanayojulikana kama “Nishati Safi Cup” Wilaya ya Mpwapwa, mkoani Dodoma lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ajenda yake ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa Watanzania wote. Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, Mratibu wa mashindano kutoka FDH Sports Promotion, Noel Simon, amesema taasisi hiyo imeamua kutumia michezo hususan mpira wa miguu kama nyenzo ya kuwaunganisha watu katika maeneo mbalimbali ya nchi ili wapate elimu ya moja kwa moja kuhusu umuhimu wa kuachana na matumizi ya nishati chafu kama kuni na mkaa na kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi kama gesi, umeme na mkaa mbadala.  Amesema kupitia mashindano hayo, FDH inatarajia kuzifikia jamii nyingi zaidi kwa urahisi na kwa njia ya burudani, jambo linalosaidia ujumbe kufika kwa haraka na kueleweka kwa urahisi.  Aidha, amebainisha kuwa ...

TUWAKATAE WANAOTAFUTA HAKI KWA KUVUNJA SHERIA,OKTOBA 29 NI SIKU YA UPIGAJI KURA NA SIO MAANDAMANO, TUSIRUBUNIWE.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam. JAMII imesisitizwa kujitokeza kwa Wingi Oktoba 29, 2025 na kupiga kura kuwachagua Viongozi wanaofaa na wanaoweza kuwaletea maendeleo ya kweli kama sehemu ya kutimiza Haki ya kila Mwananchi Kikatiba lakini pia katika kuamua hatma ya maisha ya Kila mmoja katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Wito huo umetolewa na Wananchi wa Tabata Jijini Dar Es Salaam leo Jumatatu Oktoba 06, 2025 wakati wakizungumza na Mwandishi wetu wa habari, wakisisitiza pia kila mmoja kufanya tafakuri na kutokubali kurubuniwa na kujiingiza kwenye maandamano yanayoratibiwa na kuhamasishwa na watu wasiokuwa nchini na wasioitakia mema Tanzania. Ally Kazimoto ni mmoja wa waliozungumza nasi ambapo ametanabainisha kujiandaa vyema kushiriki katika uchaguzi Mkuu ujao na kuhamasisha Vijana wenzake kutorubuniwa kuandamana, akisema ni muhimu kabla ya kuandamana kujiuliza athari za maandamano hayo,akisisitiza kuwa haki haidaiwi kwa kuvunja sheria na miongozo iliyopo nchini. Kwa upande wa...

WANANCHI BUNDA WAISHUKURU SERIKALI UJENZI WA VIZIMBA KUZUIA MAMBA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Bunda. WANANCHI wa Wilaya ya Bunda mkoani Mara wameipongeza na kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kwa kuwajengea vizimba vya kuzuia mamba kuwadhuru wakati wa kuchota maji ziwani na kufanya shughuli zingine pembezoni mwa Ziwa Victoria ikiwemo kufua na kuoga. Wamesema hayo leo Oktoba 6, 2025 kwa nyakati tofauti wakati timu ya wataalam kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ilipotembelea maeneo ya vizimba hivyo. Akizungumza katika ziara hiyo,Mkazi wa Mwiseni,kata ya Butimba, Bi. Gabaseki Gervaz  amesema wamefurahi sana kupata kizimba kutokana na changamoto walizokuwa wanakutana nazo mwanzoni za kukamatwa na mamba wanapofanya shughuli zao pembezoni mwa ziwa. "Serikali baada ya kuona tunateseka kutokana na vifo kila mwaka kwa kuuliwa na mamba ikajenga kizimba hiki" amesema Bi. Gervas na kuiomba Serikali kuongeza vizimba vya ziada kwa ajili ya jinsia ya ki...

POLISI YAONYA WANAOHAMASISHA UVUNJIFU WA AMANI KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII

Picha
Na Hamida Ramadhani, Dodoma. JESHI la Polisi nchini Tanzania limewahakikishia watanzania wote kuwa litaendelea kuwasaka, kuwakamata na kuwafikisha katika Mamlaka nyingine za haki Jinai wale wote ambao kupitia Mitandao mbalimbali ya Kijamii wamekuwa na tabia ya kutengeneza, kuandika na kusambaza maandishi na picha mjongeo za kuhamasisha watu kufanya vitendo vya kihalifu ambavyo vimekuwa ni kinyume na maadili na utamaduni wa Mtanzania ikiwa pia ni kinyume na sheria za nchi. Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania DCP David Misiime imeeleza kuwa vitendo hivyo vinasukumwa na dhamira ovu ambapo pamoja na kwamba ni kinyume cha sheria za nchi, vimekuwa vikisababisha hofu na taharuki kwa wananchi wema walio wengi kuliko wao wenye nia Ovu bila ya kuwa na sababu zozote za msingi. "Jeshi la Polisi linaendelea kuwahakikishia Watanzania kuwa linaendelea kuwasaka na kuwakamata na kuwafikisha katika Mamlaka nyingine za haki jinai kwa hatua za kisheria kama ambavyo limes...

WAZIRI NDUMBARO ATEMBELEA MAZOEZI YA STARS

Picha
WAZIRI wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro, ametembelea mazoezi ya Timu ya Taifa Stars @taifastars_ yaliyofanyika uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa kufuzu kombe la Dunia 2026 dhidi ya Zambia utakaochezwa Oktoba 8, 2025 Amaan, Zanzibar. (Picha kwahisani ya TFF)