Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba 13, 2025

ZAIDI YA LESENI 700 ZATOLEWA KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Mahenge - Morogoro. KATIKA kipindi cha miaka mitatu kuanzia Mwaka 2022 hadi 2025 zimetolewa  leseni  714 katika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mahenge zikijumuhisha leseni za  utafiti, uchimbaji na biashara ya madini kwa wadau mbalimbali wanajishughulisha na uwekezaji katika Sekta ya Madini. Hayo yalielezwa Novemba 12, 2025 na Afisa Madini Mkazi , Mkoa wa Kimadini Mahenge Jonas Mwano wakati akielezea kuhusu mafanikio yaliyopo. Mwano alisema kuwa, mafanikio hayo miaka mitatu yamepelekea kufikia lengo la ukusanyaji wa  maduhuli kwa asilimia 78.7 katika wilaya ya Ulanga, Malinyi na Kilombero. Aidha katika kipindi cha mwezi Julai mpaka Oktoba 2025 Ofisi imekusanya asilimia 61 ya lengo katika kipindi  husika. Akielezea kuhusu aina ya leseni zilitolewa Mwano alifafanua kuwa, katika kipindi husika kulitolewa aina mbalimbali za  leseni  kama leseni za utafiti 15, leseni kubwa ya uchimbaji 2, leseni ndogo ya uchimbaji 277, leseni kubwa ya...

JUKWAA LA NASSER LA KIMATAIFA LA SHEREHEKEA KISWAHILI KUTABULIWA RASMI NA UNESCO.

Picha
  Na Mwandishi Wetu. JUKWAA la Nasser la Kimataifa lisherehekea Kutambulishwa kwa Kiswahili Kama Lugha Rasmi ya UNESCO na Kuimarisha Umaarufu Wake Ulimwenguni. Jukwaa la Nasser limekumbushwa kwa sherehe katika taarifa yake kufuatia tangazo la Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) la kutambulisha Kiswahili rasmi kama mojawapo ya lugha za kazi katika mikutano mikubwa ya shirika hilo, wakati wa Kikao cha 43 cha Bunge Kuu kilichofanyika Samarkand – Uzbekistan kuanzia Oktoba 30 hadi Novemba 13, 2025. Uamuzi huu wa kihistoria ulitokana na ombi lililotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa ushirikiano na Baraza la Kiswahili BAKITA na BAKIZA, ambapo Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Mwakilishi wa Kudumu kwa UNESCO, Ali Jaberi Madini, alitoa hotuba ya nchi baada ya uamuzi huo kutambulishwa rasmi. Aidha, Jukwaa hilo limebainisha katika taarifa yake kwamba kwa mafanikio haya, Kiswahili ki...

TAARIFA KWA UMMA

Picha