Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 17, 2026

SERIKALI YAENDELEA KUTENGA MAENEO NA KUTOA LESENI KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI

Picha
Na Hamida Ramadhan,  Dodoma MKURUGENZI wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira kutoka Tume ya Madini, Hamisi Kamando, amesema serikali inaendelea kutenga maeneo maalum kwa ajili ya wachimbaji wadogo wa madini, kuwapatia leseni na kuwaendeleza ili waweze kunufaika na rasilimali za madini. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma, Mhandisi Kamando amesema kuwa kupitia Wizara ya Madini, serikali imeendelea kutenga maeneo ya uchimbaji wa madini kwa wachimbaji wadogo nchini, ambapo hadi sasa jumla ya maeneo 65 yamependekezwa kutengwa kwa ajili ya kugawiwa kwa wananchi. Amesema maeneo hayo yapo katika mikoa mbalimbali ya kimadini ikiwemo Mtwara, Manyara, Lindi, Morogoro, Dodoma, Tabora, Pwani, Tanga, Geita, Shinyanga, Mwanza, Mara, Mbeya na Ruvuma. Aidha amesema katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2025, serikali ilitoa jumla ya leseni 5,983 za uchimbaji mdogo wa madini, sawa na asilimia 71 ya leseni zote zilizotolewa katika kipindi hicho, ambapo leseni hizo hutolewa kwa Watanzani...