Na Hamida Ramadhan, Dodoma WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka waajiri wa taasisi za umma kuhakikisha wanalipa stahiki za madereva kwa wakati, kutoa mafunzo ya mara kwa mara, kutekeleza ipasavyo miundo ya ajira na kuwapa motisha ili kuongeza tija katika utendaji kazi wao. Akizungumza jijini Dodoma wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania (CMST), Waziri Mkuu amesema madereva wa Serikali wana mchango mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Serikali na hivyo wanapaswa kuheshimiwa na kuthaminiwa. "Waajiri mnapaswa kuhakikisha madereva wanalipwa stahiki zao kwa wakati, wanapewa mafunzo stahiki na kuzingatiwa katika motisha mbalimbali. Hii itawajengea morali na kuongeza ufanisi katika kazi zao," amesema Majaliwa. Aidha, amesisitiza kuwa madereva wanawajibu wa kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu, ikiwa ni pamoja na kuhakiki usalama wa vyombo vya usafiri, abiria, mizigo na nyaraka za Serikali. “Madereva mnatakiwa kufanya...