Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 19, 2025

KESI YA LISSU YAPELEKWA MAHAKAMA KUU.

Picha
Na Lubango Mleka, Dar es Salaam.  KESI ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, sasa imepelekwa Mahakama Kuu. Hatua hiyo imekuja baada ya Hakimu Franco Kiswaga jana kubaini kuwa Lissu ana kesi ya kujibu, katika shauri lililosomwa kwa takribani saa 8 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.  Lissu anatuhumiwa kwa kosa la uhaini, kinyume na kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, akidaiwa kulitenda Aprili 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam.  Katika usikilizwaji wa jana, mashahidi 30 walitoa ushahidi wao. Hata hivyo,mara baada ya mwenendo wa kesi hiyo,  mjadala mkubwa umeibuka kuhusu uamuzi wa mahakama kupiga marufuku urushaji wa moja kwa moja wa kesi hiyo. Endelea kutuatilia habarikamilitv.blogspot.com 

WANANCHI RORYA WAHIMIZWA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Rorya Mara.  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndugu Ismail Ali Ussi amewahimiza wananchi wa Wilaya ya Rorya kutumia nishati safi ya kupikia katika maeneo yao kutokana na faida mbalimbali zinazopatikana kwa kutumia nishati safi.  Akizungumza na wananchi katika Shule ya Sekondari Nyamunga, baada ya kutembelea mradi wa nishati safi wa shule hiyo, Ndugu Ussi amesema kwa kupikia nishati safi wananchi watapika kwa gharama nafuu na pia watakuwa wanatunza mazingira.  “Nishati safi inasaidia sana kwani gharama zake ni nafuu, haiathiri afya ya mtumiaji kama ilivyo katika matumizi ya kuni na mkaa na inasaidia kutunza mazingira yanayotuzunguka, hivyo ni muhimu sisi sote kutumia nishati safi majumbani mwetu” amesema Ndugu Ussi.  Ndugu Ussi ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Rorya kwa kuwekeza fedha shilingi milioni 11 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo katika Shule ya Sekondari Nyamunga ambao amesema unalinda afya za wapishi na mazingira ya Halmashauri hiyo...

HANDENI MJI YAJA NA MWAROBAINI WA UTORO SHULENI.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Handeni HALMASHAURI ya Mji Handeni, mkoani Tanga kupitia Idara ya Elimu Msingi imepongezwa kwa kubuni mkakati maalum unaoongeza uwajibikaji wa wazazi katika kukabiliana na utoro shuleni. Pongezi hizo zimetolewa Agosti 18, 2025 mjini hapa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, Mhe. Salum Nyamwese katika kikao na Menejimenti ya Halmashauri hiyo (CMT). Amesema mkakati huo unaongeza ushiriki wa wazazi na viongozi wa mtaa na kata katika kufuatilia kwa karibu maendeleo ya wanafunzi ili kudhibiti utoro kwa shule za msingi na kwamba ubunifu huo pia utafanyika kwa shule za sekondari. Amesisitiza watumishi wa halmashauri hiyo kuwa wabunifu katika utendaji kazi wao ili wananchi waendelee kupata huduma bora. Pamoja na hayo, Nyamwese amehimiza uwajibikaji, ushirikiano na kujiepusha kufanya kazi kwa mazoea ili matokeo yaonekane kwa wananchi. “Hakikisheni mnaweka mbele maslahi ya wananchi na taifa kwa kutoa huduma bora kwa wananchi wetu, sisi ni rasilimali ya umma kutokana na ...