KESI YA LISSU YAPELEKWA MAHAKAMA KUU.
Na Lubango Mleka, Dar es Salaam.
KESI ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, sasa imepelekwa Mahakama Kuu. Hatua hiyo imekuja baada ya Hakimu Franco Kiswaga jana kubaini kuwa Lissu ana kesi ya kujibu, katika shauri lililosomwa kwa takribani saa 8 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Lissu anatuhumiwa kwa kosa la uhaini, kinyume na kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, akidaiwa kulitenda Aprili 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Katika usikilizwaji wa jana, mashahidi 30 walitoa ushahidi wao. Hata hivyo,mara baada ya mwenendo wa kesi hiyo, mjadala mkubwa umeibuka kuhusu uamuzi wa mahakama kupiga marufuku urushaji wa moja kwa moja wa kesi hiyo.
Endelea kutuatilia habarikamilitv.blogspot.com

Maoni