Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili 25, 2026

DC MYINGA ATOA AGIZO ZITO KWA VIONGOZI SIKONGE JUU YA UPUNGUFU WA MADAWATI KWA SHULE ZA MSINGI.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Sikonge-Tabora.  UPUNGUFU wa madawati katika shule za msingi Wilayani Sikonge umechukua sura mpya baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Mheshimiwa Thomas Myinga, kutoa agizo kali kwa viongozi wa vijiji na kata kuhakikisha wanatumia rasilimali zilizopo kumaliza changamoto hiyo kwa haraka. Akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha viongozi wa serikali za vijiji, kata pamoja na walimu, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Mheshimiwa Myinga alisisitiza kuwa hakuna sababu ya wanafunzi kuendelea kukaa chini ilhali maeneo yao yana rasilimali za kutosha, ikiwemo misitu inayoweza kutumika kutengeneza madawati. Alielekeza viongozi hao kupanga na kutekeleza bajeti zao kwa kuzingatia kipaumbele cha elimu, akibainisha kuwa ushirikiano kati ya serikali, wananchi na wadau wa maendeleo ni muhimu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora ya kujifunzia. Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Seif Salum...

SERIKALI YAJA NA MKAKATI MPYA WA KULINDA FEDHA ZA USHIRIKA

Picha
  Na Jasmine Shamwepu, Dodoma.  SERIKALI imezindua mkakati mpya wa kuimarisha usimamizi wa vyama vya ushirika nchini, ukiwa na lengo la kulinda fedha za wanachama na kuongeza uwajibikaji kwa viongozi. Akizungumza jijini Dodoma katika Mkutano wa Wadau wa Maendeleo ya Ushirika, Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo, amesema kuwa sekta ya ushirika ina mchango mkubwa katika uchumi wa taifa, ikizingatiwa kuwa inazungusha fedha zinazokadiriwa kufikia trilioni sita. Amesema kuwa ili kuhakikisha fedha hizo zinalindwa ipasavyo, serikali inapanga kuimarisha mifumo ya ukaguzi, usimamizi na uwazi, sambamba na kuanzisha miundombinu maalum ya kushughulikia makosa yanayohusiana na vyama vya ushirika. “Lengo letu ni kuona vyama vya ushirika vinakuwa salama, vinawanufaisha wanachama, na vinaendeshwa kwa uadilifu mkubwa,” amesema Chongolo. Katika hatua nyingine, serikali imeweka mkazo katika matumizi ya teknolojia ya kidijitali ili kurahisisha ufuatiliaji wa shughuli za kifedha, kuongeza uwazi...