Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 20, 2026

HALMASHAURI YA JIJI LA DAR KURASIMISHA SHUGHULI ZA WACHAKATAJI TAKA KUJIINUA KIUCHUMI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam.  HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha uchumi wa Wananchi kwa kurasimisha shughuli za wachakataji wa taka rejea. Kupitia kikao kilichofanyika tarehe 18 Machi 2026,  katika ukumbi mdogo wa meya Jijini Dar es salaam. wadau wamepewa mwongozo wa namna ya kufanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria, ikiwemo usajili na upatikanaji wa leseni za biashara. Hatua hii inalenga kufungua fursa zaidi za ajira kwa vijana na wanawake, kulinda mazingira, na kuongeza kipato kwa wajasiriamali wadogo. Aidha, urasimishaji huu utawezesha upatikanaji wa elimu, teknolojia na masoko bora, hivyo kuchangia maendeleo endelevu ya jiji.

CCM SIMANJIRO WAENDELEA NA ZIARA

Picha
  Na Mwandishi wetu, Simanjiro.  SEKTRETARIETI ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, imeendeleza na ziara ya kata mbalimbali ili kushukuru, kusikiliza kero na kukagua uhai. Katibu wa CCM Wilaya ya Simanjiro, Wambura Igembya ameongoza wajumbe wa sekretarieti hiyo katika ziara ya kutembelea kata hizo. Wambura ameongozana na wajumbe wa sekretarieti ya CCM ya Wilaya hiyo, akiwemo Katibu Mwenezi Mosses Makeseni, Katibu wa Wazazi Sasi Mirumbe na Katibu wa UWT Tichomo Sangija Amesema lengo la ziara hiyo ni kuwashukuru wana Simanjiro kwa kuichagua CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2026, kusikiliza kero zao na kukagua uhai wa chama. "Tunawashukuru wana Simanjiro kwa kumpa kura nyingi za kishindo Rais Samia Suluhu Hassan, kumchagua mbunge kwa tiketi ya CCM James Ole Millya ambaye ameteuliwa na Rais kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kuwachagua madiwani wa CCM," amesema Wambura. Amesema katika ziara hiyo wataanza kwa kuzite...

NKINGA HOSPITALI YAOKOA MAISHA YA MAMA ALIYEPATA TATIZO LA KUJIFUNGUA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Nkinga - Igunga.  IDARA ya Wanawake na Uzazi katika Hospitali ya Rufaa ya Nkinga imefanikiwa kuokoa maisha ya bi. Mbalu Jisinza (45), mkazi wa kijiji cha Mwanzugi wilayani Igunga, aliyepata tatizo hatari la kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua, hali iliyohatarisha maisha yake kabla ya kupatiwa matibabu ya haraka na ya kibingwa hospitalini hapo. Akizungumza wakati anapatiwa matibabu Hospitalini hapa Bi.Jisinza amesema, anachokumbuka mara ya mwisho alikuwa kwenye kituo cha afya kwaajili ya kujifungua, ambapo alijifungua mtoto mfu kisha akaanza kutokwa na damu nyingi, juhudi za madaktari kuzuia  tatizo la kutokwa na damu zilishindikana wakamfanyia upasuaji wa kuondoa kizazi, lakini bado damu zilikuwa zinatoka. Akiwa kituoni hapo alianza kushindwa kupumua wakamuwekea mpira wa Oxygen akiwa hajitambui, alipata fahamu akiwa chumba cha (ICU) hapa Nkinga Hospitali, Bi.Mbalu amewashukuru madaktari na Wauguzi wa Nkinga Hospitali kwa huduma nzuri waliyompat...

MHUBIRI WA KIMATAIFA DKT DANA MOREY AWASHA MOTO WA INJILI TABORA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora.  WAKAZI wa Manispaa ya Tabora na Mikoa jirani wamemiminika kwenye mkutano mkubwa wa injili unaohubiriwa na Mwinjilisti wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Dkt Dana Morey ulioanza jana Mjini Tabora na kupokea baraka na uponyaji. Wakizungumza baada ya kuombewa na Mwinjilisti huyo wameeleza kufurahishwa na uamuzi wa Serikali ya Mkoa kuruhusu mkutano huo uendelee baada ya awali kuuzuia kwa kile kilichoelezwa kuwa wanagwa vitu visivyo na maadili kwa jamii. Mkazi wa kata ya Tambuka-Reli katika Manispaa hiyo Magreth Lutaha (60) amweleza kuwa alikuwa na tatizo la uoni hafifu kwa zaidi ya miaka 10 lakini baada ya kuombewa na Mwinjili huyo amepokea uponyaji na sasa anaona vizuri. ‘Namshukuru Mungu nilikuwa sioni vitu vya mbali na kichwa kilikuwa kinaniuma kwa muda mrefu sana ila baada ya maombi kichwa hakiumi tena na sasa naona hata vitu vya mbali’, amesema. Mariam Mayani (40) mkazi wa Nzega na Furaha Jungu (30) mkazi wa Kiloleni katika manispaa ya Tabora wamee...