HALMASHAURI YA JIJI LA DAR KURASIMISHA SHUGHULI ZA WACHAKATAJI TAKA KUJIINUA KIUCHUMI

 


Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam. 

HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha uchumi wa Wananchi kwa kurasimisha shughuli za wachakataji wa taka rejea. Kupitia kikao kilichofanyika tarehe 18 Machi 2026,  katika ukumbi mdogo wa meya Jijini Dar es salaam.

wadau wamepewa mwongozo wa namna ya kufanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria, ikiwemo usajili na upatikanaji wa leseni za biashara.

Hatua hii inalenga kufungua fursa zaidi za ajira kwa vijana na wanawake, kulinda mazingira, na kuongeza kipato kwa wajasiriamali wadogo. Aidha, urasimishaji huu utawezesha upatikanaji wa elimu, teknolojia na masoko bora, hivyo kuchangia maendeleo endelevu ya jiji.













Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.