MWENYEKITI MAREMA AWASIHI WACHIMBAJI KUSAIDIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO
Na mwandishi wetu, Mirerani. MWENYEKITI wa chama cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara (MAREMA) Elisha Nelson Mnyawi amewaomba wadau wa madini kujitolea na kuwasaidia waathirika wa mafuriko katika Tarafa ya Moipo. Mwenyekiti huyo wa MAREMA Mnyawi ameyasema hayo mji mdogo wa Mirerani, leo jumapili Machi 29,2026 wakati akikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mwalimu Fakii Raphael Lulandana vyakula na vifaa vya thamani ya shilingi milioni 22 vilivyotolewa na kampuni ya Permanent Mining LTD kwa ajili ya waathirika wa mafuriko katika Tarafa ya Moipo. Ameeleza kuwa japokuwa wachimbaji madini wamekuwa wakijitoa mara kwa mara kupitia hisani kwa jamii (CSR) wasiliache hilo likapita bila kuchangia chochote. Amesema wachimbaji mbalimbali ikiwemo Franone Mining, God Mwanga, Chusa Mining, California Camp, Bilionea Saniniu Laizer, Sunda Mining wamekuwa wakisaidia jamii wasaidie pia waathirika hao waliokumbwa na mafuriko. "Kupitia hadhara hii nampongeza Mkurugenzi wetu God Charity amba...