Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 11, 2025

JESHI LA POLISI LATAKIWA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA WADAU WA UCHAGUZI NCHINI.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Moshi.  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema ni muhimu Jeshi la Polisi kuimarisha ushirikiano wa karibu na wadau wote wa uchaguzi, hatua ambayo itasaidia kuhakikisha kila mdau anatendewa haki, na kuondoa tofauti zinazoweza kusababisha migongano.   Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Polisi (CCP) Moshi Mkoani Kilimanjaro. Amesema Baadhi ya maeneo muhimu ya ushirikiano ni pamoja na kuhakikisha mikutano ya kampeni inafanyika kwenye maeneo yaliyoruhusiwa na ndani ya muda uliopangwa,  Kuzuia maandamano yasiyo na kibali, kuimarisha ulinzi wa wagombea na viongozi wa vyama vya kisiasa, bila kujali vyama vyao au itikadi zao pamoja na kudhibiti misongamano mikubwa ya watu ili kuhakikisha shughuli nyingine za kijamii na kiuchumi zinaendelea bila usumbufu.   Pia Makamu wa Rais amelitaka Jeshi la Polisi ku...

RAIS MWINYI ATEMBELEA ENEO LA OFISI ZA MJI WA SERIKALI NA LINALOJENGWA UWANJA MPYA WA AFCON

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameeleza kuwa Serikali inaendelea kusimamia utekelezaji wa mradi mkubwa wa uwanja wa AFCON pamoja na miundombinu mbalimbali inayojengwa Fumba, hivyo ni muhimu kubaini mapema maeneo yatakayotumika kwa mradi huo ili kuepusha mwingiliano wa matumizi ya ardhi katika eneo hilo kati ya taasisi husika. Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 11 Agosti 2025, katika kikao maalum na mawaziri mbalimbali akiwemo Mhe. Rahma Kassim Ali, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, Mhe. Shariff Ali Shariff, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mhe. Tabia Maulid Mwita, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, pamoja na Taasisi ya Ofisi ya Rais, Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (ZPDB), kwa lengo la kupata uelewa wa pamoja kuhusu matumizi sahihi ya ardhi katika maeneo ya uweke...

MADEREVA, ABIRIA WAPATIWA ELIMU YA USALAMA BARABARANI NA MATUMIZI SAHIHI YA VYOMBO VYA KUZIMIA MOTO IGUNGA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Igunga.  MADEREVA na Abiria katika Kituo cha Mabasi Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora wamepatiwa Elimu ya Usalama Barabarani na Mabalozi wa Usalama Barabarani Wilaya ya Igunga (RSA) yenye lengo la kuendelea kuwakumbusha Madereva na Abiria kufuata sheria za usalama barabarani ili kunguza ajali zitokanazo na ubovu wa magari na uzembe wa Madereva.  Elimu hiyo imetolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la Road Safety Ambassadors (RSA) kwa kushirikiani na Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani na Jeshi la Zimamoto wilaya ya Igunga ambapo wametoa Elimu ya Usalama Barabarani, Wajibu na Haki za Abiria, Elimu ya tahadhari  ya majanga ya Moto pia imbeambatana na zoezi la ukaguzi wa magari, vifaa vya kuzimia moto na ukaguzi wa leseni kwa madereva.  Akitoa Elimu ya tahadhari ya majanga ya moto Koplo Shadrack Mweya kutoka Jeshi la Zimamoto amewataka madereva kuhakikisha magari yao yanakuwa na vifaa vya kuzimia moto ambavyo havijaisha muda wa matumizi, milan...