Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba 23, 2025

USAFIRI WA SGR DAR ES SALAAM- DODOMA WAREJEA, TRC YAOMBA RADHI KWA USUMBUFU

Picha
  Na Hamida Ramadhani, Dodoma. SHIRIKA la reli Tanzania limeufahamisha umma wa Watanzania kuwa huduma za usafiri wa treni za SGR zimerejea na kuendelea kama kawaida, likiomba radhi kwa wateja wake kwa usumbufu uliojitokeza, shirika likiwashukuru pia Wananchi kwa uvumilivu wao katika kipindi ambacho huduma za usafiri huo zilipotatizika kutokana na hitilafu iliyotokea mapema leo Alhamisi Oktoba 23, 2025. Mapema leo Shirika la Reli Tanzania lilitoa taarifa kwa Vyombo vya habari likieleza kuhusu ajali ya Treni ya EMU iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar Es Salaam kwenda Dodoma majira ya saa mbili asubuhi kutokana na hitilafu za uendeshaji, tukio ambalo lilitokea Kituo cha Ruvu na kwa taarifa za shirika hilo hakukuwa na athari kubwa za ajali hiyo. Timu ya wataalamu ikiongozwa na Katibu Mkuu wa uchukuzi, Mkurugenzi wa shirika la TRC, Vyombo vya ulinzi na usalama na menejimenti ya TRC ilianza haraka kushughulikia changamoto hiyo na kufanya uchunguzi wa kina wa kuhakikisha kuwa huduma hizo zimer...

DKT.ABBASI, MWAKILISHI MKAZI UNDP WAZINDUA UBORESHAJI MISITU NCHINI.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam. SERIKALI imezindua rasmi utekelezaji wa mradi mkubwa wa kimataifa wa mazingira ujulikanao kama “Mbinu Chanya na Jumuishi za Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi na Kulinda Bayoanuai” (Integrated Net-Zero Nature-Positive Solutions for Climate and Biodiversity Protection), unaolenga kuendeleza sekta ya misitu kwa lengo la kuinua maisha ya watu. Akizungumza leo Oktoba 23,2025 jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kikao cha kwanza cha Kamati ya Usimamizi wa Mradi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, ambaye ni Mwenyekiti alisema mradi huo wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 38 ni uthibitisho wa kuaminiwa kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. “Mradi huu ni ushahidi wa juhudi za Serikali katika kulinda mazingira, kuhifadhi misitu na kuhamasisha nishati safi. Dunia inatambua uongozi wa Tanzania katika masuala ya uchumi wa kijani ndio maana baadhi ya wadau wa Mradi huu pamoja ...

TAARIFA KWA UMMA

Picha

REA YAENDELEA KUTEKELEZA KWA VITENDO MKAKATI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Picha
Majiko banifu 4,836 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoa wa Njombe. Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 8,850 tu,Kila walaya kupata majiko 1,209 Na Lunango Mleka, Njombe. MKUU wa  Wilaya ya Ludewa Mhe. Olivanus Thomas akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka leo Oktoba 20,2025 amezindua rasmi mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku mkoa wa Njombe. uzinduzi huo umeongozwa na mkuu wa wilaya , Maafisa kutoka REA pamoja na viongozi wengine wa mkoa, wilaya, kata, vijiji na vitongoji vyake.  Mhe. Olivanus amesema , lengo la uzinduzi  wa mradi huu ni kuutambulisha rasmi mradi kwa wananchi wa mkoa wa Njombe ambao ndio walengwa na wanufaika wa mradi. Mhe. Olivanus, amepongeza juhudi za Serikali na REA katika kufanikisha utekelezaji wa mradi na kuongeza kuwa lengo la Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia ni kuwa ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, jambo ambalo litasaidia kutunza Afya...