Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba 5, 2025

DOROTHY SEMU: MWAROBAINI WA HUDUMA ZA AFYA NI KUICHAGUA ACT-WAZALENDO

Picha
Na Mwandishi Wetu, Kilosa -Morogoro. KIONGOZI wa Chama Cha ACT Wazalendo, Ndugu @dorothysemu  leo 05 Oktoba, 2025 amefanya Mkutano wa hadhara wa kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo Ndugu, Hassan Mbaruku Thabiti pamoja na wagombea Udiwani. Kiongozi wa Chama, Dorothy Semu Katika hotuba yake amewaeleza Wana Kilosa juu ya huduma za Afya muarobaini ni kuichagua ACT Wazalendo ambapo jawabu letu ni kufuta Bima ya Afya kwa wote yenye vifurushi na kuwapa watanzania Bima ya Afya kwa wote isiyo na Vifurushi. Ameongeza zaidi na kusema "Tunakataa Watanzania kubaguliwa katika mifumo ya Afya kwa uwezo wao, tunataka watu wote wajumuishwe na wapate huduma bora za Afya bila kujali tabaka lake la kipato" KC, Dorothy Semu juu ya migogoro ya ardhi amewaeleza watu wa kilosa kwamba "Uongozi wa Serikali ya CCM umeshindwa kutatua kero hii ya migogoro ya Ardhi badala yake wamezidi kuchochea na kila kona kukutana na changamoto hii.  Ameongeza kuwa, "ACT Wazalendo juu ya hili tunasema tunatak...

TAARIFA KWA UMMA

Picha
  Shauri la Ndugu Luhaga Joelson Mpina dhidi ya Tume Huru ya Uchaguzi kusikilizwa kesho Oktoba 6, 2025 Mahakama Kuu Masjala ya Dodoma. #Oktoba #LindaKura #TunapambanaTukishiriki

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA SUDANI KUSINI AMEFANYA ZIARA KWA MARA YA KWANZA NCHINI SUDANI.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Port Sudani. WAZIRI wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Sudani Kusini, Mhe. Jumatatu Semaya, amefika Port Sudan kwa ziara rasmi ya siku mbili-ziara yake ya kwanza nchini Sudan tangu kudhani ofisi-ililenga kuimarisha uhusiano wa nchi mbili na kuchunguza maeneo mapya ya ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili ya ndugu huku kukiwa na changamoto za kikanda.  Akiwa kwenye uwanja wa ndege wa Port Sudan, Waziri Semaya amepokelewa na Waziri wa Mambo ya nje wa Sudan, Amb. Mohy Eldin Salem, pamoja na maafisa wakuu kutoka Wizara na Chargé D'Asha ya Ubalozi wa Sudani Kusini.  Wakati wa ziara yake, Waziri Semaya amepanga kukutana na maafisa kadhaa wakuu wa Sudan kujadili ushirikiano katika uwanja wa kisiasa, kiuchumi, na usalama, na kuimarisha uratibu kati ya Juba na Khartoum.  Ziara hii inasisitiza kujitolea kwa Juba katika kukuza uhusiano wa kindugu na kuendeleza juhudi za pamoja za amani, utulivu, na kufanikiwa kati ya Sudani Kusini na Sudan...

DKT.MWINYI: TUMEONDOA UBAGUZI NA KUJENGA UMOJA WA WAZANZIBARI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar. MGOMBEA wa nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuondoa ubaguzi, mifarakano na siasa za chuki katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Akizungumza katika mkutano na viongozi wa dini, masheikh, watawa na mapadri uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Utaani, Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, leo tarehe 05 Oktoba 2025, Dkt. Mwinyi amesema kuwa umoja wa Wazanzibari ndio nguzo kuu ya mafanikio ya Serikali na maendeleo ya Taifa. Ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Nane chini ya CCM imefanikiwa kuimarisha maridhiano, umoja wa kitaifa na kuondoa ubaguzi katika nafasi na majukumu ya kitaifa, kwa maslahi ya wananchi wote. Rais Dkt. Mwinyi amesema mafanikio makubwa yamepatikana katika sekta za elimu, afya, ustawi wa jamii, huduma za maji na miundombinu, akisisitiza kuwa Serikali tayari im...

MWENYEKITI WA BODI YA ARAB CONTRACTORS AKAGUA MRADI WA BWAWA LA JULIUS NYERERE.

Picha
Mwenyekiti wa Bodi ya Arab Contractors akagua Mradi wa Bwawa la "Julius Nyerere" Nchini Tanzania Kuimarisha Ushirikiano kati ya Misri na Tanzania. MHANDISI Ahmed Al-Assar, Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Arab Contractors, na Mhandisi Wael Hamdy, Naibu Mwenyekiti wa Elsewedy Electric Group, wamefanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa bwawa na kituo cha umeme cha Julius Nyerere nchini Tanzania, unaotekelezwa na makampuni hayo mawili ya Misri kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania.  Ziara hii inakuja kama sehemu ya juhudi za kuimarisha mahusiano kati ya Misri na Tanzania, na kufuatilia utekelezaji wa mradi huu mkubwa unaoonesha ukina wa ushirikiano kati ya mataifa haya mawili na dhamira ya Misri ya uungaji mkono juhudi za maendeleo barani Afrika, hasa katika sekta za miundombinu na nishati. Mradi huu ni miongoni mwa miradi mikubwa zaidi barani Afrika, wenye lengo la kuzalisha megawati 2115 za umeme na kudhibiti mafuriko ya Mto Rufiji, jambo litakalochangia kulinda mazingi...

RAIS MWINYI AAHIDI KUENDELEA KUWAJENGEA UWEZO WALIMU NA KUIIMARISHA SEKTA YA ELIMU

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kuimarisha sekta ya elimu, maslahi na mazingira ya kazi ya walimu ili kuwaongezea ari na motisha katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi. Akihutubia katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani, yaliyofanyika katika Viwanja vya Polisi Ziwani, Mkoa wa Mjini Magharibi, Dkt. Mwinyi amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa walimu katika maendeleo ya taifa na malezi ya vijana kielimu. Ameeleza kuwa walimu ni fahari ya familia, taifa na jamii kwa ujumla, na ni daraja la kuifikisha jamii kwenye maarifa. Kwa msingi huo, Serikali imeiweka sekta ya elimu miongoni mwa sekta za kipaumbele kutokana na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya sekta nyingine zote. Rais Dkt. Mwinyi amewahakikishia walimu kuwa Serikali itaendelea kutoa ajira mpya kwa walimu kila mwaka, sambamba na kuboresha maslahi yao ikiwemo posho za ku...

DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AHUDHULIA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.

Picha
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi alipozungumza katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani, yaliyofanyika katika Viwanja vya Polisi Ziwani, Mkoa wa Mjini Magharibi, leo tarehe 5 Oktoba 2025.

MGOMBEA URAIS CCM AFANYA MIKUTANO 21, AZIDI KUNADI SERA KWA HESHIMA NA UTULIVU

Picha
Na Mwandishi Wetu,Dodoma. CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuwa mgombea wake wa nafasi ya Urais tayari amefanikisha mikutano zaidi ya 21 ya kampeni katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar, akiwa katika harakati za kunadi sera za chama hicho kwa njia ya kistaarabu, yenye kuzingatia maadili, utu na mshikamano wa kitaifa. Kauli hiyo imetolewa leo, Oktoba 5, 2025, jijini Dodoma na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa kampeni zinazoendelea kufanywa na mgombea huyo kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni. Kihongosi amesema kuwa ziara hizo zimekuwa chachu ya matumaini kwa Watanzania, kwa kuwa zimejikita katika kuelezea vipaumbele vya maendeleo ya nchi, ikiwa ni pamoja na kuboresha uchumi, elimu, afya, miundombinu na ajira kwa vijana. “Mgombea wetu anaendelea kusikiliza kero za wananchi kwa karibu, na kutoa majibu ya sera zinazotekelezeka. Amekuwa mstari wa mbele kuonyes...

JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF) LAPONGEZA JWTZ KWA HATUA ILIZOCHUKUA JUU YA VIDEO INAYOHUSISHA JESHI NA SIASA.

Picha
JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limepongeza hatua za haraka zilizochukuliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kukemea video na taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya jamii zinazohusisha jeshi hilo na siasa.

TANZANIA NA KENYA KUONDOA VIKWAZO VISIVYO VYA KIUSHURU KUIMARISHA BIASHARA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam. TANZANIA na Kenya zimeahidi kuendelea kuondoa vikwazo visivyo vya kiushuru katika biashara baina yao na kuvigeuza kuwa fursa za kukuza uchumi.  Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wa Tanzania, Dkt. Hashil Abdallah, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 9 wa Kamati ya Pamoja ya Biashara uliofanyika Dar es Salaam.  Amesema biashara ndiyo msingi wa mahusiano kati ya nchi hizo, kupitia kuongeza ajira, kujenga viwanda na kuhamasisha ubunifu wa wajasiriamali ili kuboresha maisha ya wananchi. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda ya Kenya, Bi. Regina Ombam, amesema Kenya na Tanzania zina mahusiano ya kihistoria, kitamaduni na kiuchumi. Huku akibainisha kuwa, uchumi wa Tanzania unaendelea kukua kwa kasi hasa katika sekta za viwanda, ujenzi na utalii,  jambo linalofungua fursa kubwa kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa Kenya. Aidha, amesisitiza kuwa nchi hizo mbili si majirani tu, bali ni m...

KURA YAKO, NGUVU YAKO! HESHIMU DEMOKRASIA KWA KUPIGA KURA!

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dr Es Salaam. UPO ushahidi madhubuti unaoonesha uwepo wa tija ya kupiga kura Katika uchaguzi Mkuu wa Tanzania licha ya uwepo wa mitazamo na kauli mbalimbali kuwa kushiriki kwenye uchaguzi huo ni kupoteza muda tofauti na uhalisia ulivyo, uchaguzi ukitajwa kama heshima, wajibu na silaha ya Kidemokrasia kote duniani. "Kupiga kura ni haki ya Kikatiba, inayomuwezesha kila Mtanzania kushiriki katika maamuzi ya nchi kwa njia ya amani, kupitia kura wananchi huamua ni nani awaongoze katika nafasi za kisiasa kama Rais, Wabunge na Madiwani na hii ni njia halali ya kushiriki katika ujenzi wa Taifa na kuhakikisha kuwa sauti ya mwananchi inasikika." Amesema Mchambuzi wa siasa Ally Said alipozungumza nasi. Kulingana na Mchambuzi huyo, wananchi wanapojitokeza kwa wingi kupiga kura wana nafasi ya kuchagua Viongozi waadilifu na wenye uwezo wa kuwaletea maendeleo, kupitia kura matatizo ya huduma duni za jamii yanaweza kushughulikiwa, Kura ikiimarisha pia misingi ya demokrasia...

WANANCHI DAR WAASWA KUTOSHIRIKI MAANDAMANO, WASISITIZWA KUJITOKEZA KUPIGA KURA OCTOBA 29

WANANCHI DAR WAONYA KUTOSHIRIKI MAANDAMANO, WASISITIZA UMUHIMU WA KUPIGA KURA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar -Es -Salaam. WANANCHI wa Mkoa wa Dar Es Salaam wamesema wapo tayari kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, wakijitenga na ushawishi unaofanywa mtandaoni wa kuwataka kuandamana na kutojitokeza kupiga kura, wakieleza kufahamu vyema umuhimu wa amani na athari za vurugu na maandamano ikiwemo vifo, majeraha na kuporomoka kwa uchumi kutokana na kukosekana utulivu wa wao kuendelea na shughuli zao za kiuchumi. Pantaleo Mushi Mkazi wa Mbezi Beach amesema anafahamu jukumu lake la Kikatiba la kupiga kura, akihamasisha Vijana wengine kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya Kikatiba kupiga kura na kuchagua Kiongozi wamtakaye, akieleza kuwa athari za kutopiga kura ni kuruhusu kuchaguliwa kwa Kiongozi asiyemtaka na kumnyima fursa Kiongozi sahihi kuweza kushika Madaraka kwa kipindi cha miaka mitano ijayo katika Ngazi ya Kata, Jimbo na kwenye Nafasi ya Urais. Kwa upande wao Said Nassor na Yusuph Ibengwe, wakazi wa Kawe, wameeleza kutofahamu lolote kuhusu maanda...