Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 7, 2026

MBUNGE AGNESS AWAFIKIA WANAWAKE WA KIKRISTO KWA KUWASHIKA MKONO

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Mara.  MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Agnes Marwa, ameungana na wanawake wa mashirika ya Kikristo katika Musoma kuadhimisha International Women's Day kwa shangwe na mshikamano mkubwa. Katika maadhimisho hayo yaliyowakutanisha wanawake wa Christian Council of Tanzania (CCT) pamoja na WAWATA wa Manispaa ya Musoma, Mheshimiwa Mbunge alitoa pongezi kwa wanawake kwa mchango wao mkubwa katika kuimarisha maadili ya jamii, familia na maendeleo ya Taifa. Akizungumza katika sherehe hizo, Mheshimiwa Agnes Marwa aliwahimiza wanawake kuendelea kushikamana, kujiamini na kutumia fursa mbalimbali za maendeleo ili kujiletea ustawi wao na jamii kwa ujumla. Katika kuonesha dhamira yake ya dhati ya kuunga mkono shughuli za wanawake na taasisi za kijamii, Mheshimiwa Mbunge alitoa mchango wa shilingi milioni 2 na laki 4 (Tsh 2,400,000) kwa ajili ya ununuzi wa tent, hatua itakayosaidia kuimarisha uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kijamii na kiroho katika Manis...