Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili 28, 2026

MATAPELI WATANO WANASWA KWA TUHUMA ZA KUIBA MILIONI 40 TABORA

Picha
Na mwandishi wetu, Tabora. Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa shilingi milioni 40 kutoka kwa mfanyabiashara Fatuma Nasoro, mkazi wa Wilaya ya Kaliua, katika tukio lililotikisa wakazi wa eneo hilo. Kwa mujibu wa taarifa za awali, watuhumiwa hao walinaswa kufuatia msako maalum ulioendeshwa kwa nyakati tofauti ndani ya mkoa huo, baada ya kubainika kuwa walikuwa wakijihusisha na vitendo vya utapeli huku wakiendelea na maisha yao ya kawaida bila wasiwasi wowote. Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Matiko Chacha, amesema miongoni mwa waliokamatwa, wawili wanaotambulika kwa majina ya Marseli Gwasima na Fred Ricardo walitumia mbinu za udanganyifu kwa kujifanya wahudumu wa kampuni ya mawasiliano ya YAS (zamani Tigo). Ameeleza kuwa kwa kutumia ujanja huo, watuhumiwa walimshawishi mfanyabiashara huyo, anayejihusisha na biashara ya khanga na vitenge wilayani Kaliua, kuwasajili laini yake, hatua iliyowapa mwanya wa kuhamisha ...

REA YATOA ELIMU YA NISHATI SAFI KWA WANANCHI KATIKA TAMASHA LA KILIMO IWAMBI MBEYA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Iwambi-Mbeya.  WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) imeendelea kutoa elimu ya matumizi ya nishati safi kwa wananchi katika Tamasha la Kilimo linalofanyika katika viwanja vya Iwambi, mkoani Mbeya. Akizungumza wakati wa tamasha hilo, Mhandisi wa Miradi kutoka REA, Ramadhani Mganga, amesema kuwa lengo la ushiriki wao ni kuwahamasisha wananchi kutumia nishati safi na salama kwa kupikia ili kulinda afya zao na mazingira. Ameeleza kuwa REA inaendelea kusambaza na kuhamasisha matumizi ya teknolojia mbalimbali za nishati safi ikiwemo majiko ya umeme, majiko ya gesi pamoja na majiko banifu, ambayo yanasaidia kupunguza matumizi ya kuni na mkaa. “Ni muhimu kwa wananchi kuelewa faida za nishati safi, si tu katika kulinda mazingira bali pia katika kuboresha afya kwa kupunguza athari za moshi unaotokana na nishati zisizo salama,” amesema Mganga. Aidha, amebainisha kuwa kupitia miradi mbalimbali inayoendelea, upatikanaji wa umeme vijijini umeimarika kwa kiwango kikubwa, hatua inayo...

WANAFUNZI WA VYUO VIKUU NA KATI WATAKIWA KUTUMIKIA JAMII KWA KUJIFUNZA SHERIA NA KUTOA MSAADA WA KISHERIA.

Picha
Na Jasmine Shamwepu Dodoma  WANAFUNZI wa vyuo vikuu na vyuo vya kati nchini wametakiwa kujitoa kwa ajili ya kutumikia jamii kwa kujifunza sheria na kutoa msaada wa sheria kwa wananchi ili kukabiliana dhidi ya dhulma, uonevu, ukatili wa kijinsia, na migogoro ya ardhi inayoongezeka kila kukicha. Akizungumza katika Mdahalo  maalum lililofanyika katika Ukumbi wa Chimwaga uliopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma, Mkurugenzi wa Huduma  za msaada wa Sheria  Ester Msambazi  kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, amesema watu wengi wanapoteza haki zao nchini kwa kutojua sheria.  Msambazi amesema lengo la Mdahalo huo ni kuwajengea uwezo wanachuo hao kuelewa masula ya kisheria na kutambua haki zao pamoja na kufahamu wapi pa kupata huduma za msaada wa kisheria wanakupambana na changamoto." "Wizara ya katiba na sheria una Jukumu la kratibu na kusimamia upatikanaji wa haki nchini hivyo inaendelea kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo Tehama ili kuhakikisha HUDUMA hizo zinawafikia wana...