Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 11, 2026

SINGIDA 0-AZAM 1 MPIRA NI MAPUMZIKO

Picha
NBCPL Ni mapumziko na mbili kibindoni…!!! HT: Dodoma Jiji 0-2 Azam FC  #NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #ImenogaZaidi #DodomaJijiFC #AzamFC #DodomaJijiAzamFC

AFRIKA KUSINI YAONGEZA WANAJESHI KUKABILIANA NA MAGENGE YA DAWA ZA KULEVYA NA MAUAJI YA RAIA.

Picha
WANAJESHI wamepelekwa katika mitaa ya mji mkubwa zaidi nchini Afrika Kusini, Johannesburg, ili kukabiliana na uhalifu unaosababisha idadi kubwa ya watu kuuawa na mapigano kati ya magenge ya dawa za kulevya   Kwa habari zaidi tufuatilie kupitia you tube @habarikamilitv, Facebook habari kamili tv na kwenye blog @habarikamilitv

SERIKALI YAPENDEKEZA KUKUSANYA NA KUTUMIA SH. TRILIONI 62.334 KWA MWAKA WA FEDHA 2026/27

Picha
  Na Mwandishi Wetu.  WAZIRI wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, (Mb), amewasilisha Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2026/27, ambapo katika kipindi hicho, inatarajia kukusanya nakutumia shilingi trilioni 62.334 kwa ajili ya matumizi ya kawaida, maendeleo na kulipia deni la Taifa. Mhe. Balozi Omar amesema hayo wakati akiwasilisha Mpango huo ambapo amesema kwenye Kamati ya Bunge zima, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, ambapo ongezeko hilo ni sawa na asilimia 10.3 ikilinganishwa na Bajeti ya Mwaka wa Fedha, 2025/26. Tukio hilo limeongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na kuhudhuriwa pia na Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azan Zungu, na viongozi waandamizi wa Serikali.

RAIS DKT. SAMIA AMUASILI MTOTO ALIYETELEKEZWA GESTI WILAYANI NZEGA

Picha
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuasili Grace Samia Suluhu, mtoto mchanga aliyetelekezwa mjini Nzega, mkoa wa Tabora.  Dkt. Samia amesema kuwa, "Kila mtoto anayezaliwa ni baraka na hazina kwa jamii, tunao wajibu ndani ya Serikali na kila mwananchi kuhakikisha tunashiriki katika malezi, ulinzi, upendo na kesho ya watoto, kwani ndiyo kesho yetu na Taifa letu."