Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari 13, 2026

WATENDAJI SOKO LA HISA DSE WATAKIWA KUWA WABUNIFU KUVUTIA WAWEKEZAJI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Bw. Peter Nalitolela, mazungumzo yaliyofanyika leo tarehe 13 Februari 2026, Dodoma. Katika Mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amewahimiza watendaji DSE kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu katika masuala ya masoko na kuendelea kuvutia uwekezaji. Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Bw. Peter Nalitolela, ameahidi kuendelea kushirikiana vema na Serikali katika kutafuta mitaji ili kuweza kusaidia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ya kufikia uchumi wa Dola za Marekani Trilioni Moja ifikapo 2050. Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ni taasisi ya kimkakati ya Taifa inayowezesha ukusanyaji na usimamizi wa mitaji ya muda mrefu kwa ajili ya kufadhili maendeleo ya uchumi wa Tanzania. DSE ni jukwaa rasmi linalowawezesha wawekezaji wa ndani na ...

DC SENDIGA AWATAKA WACHIMBAJI KUCHANGAMKIA BIMA YA AFYA

Picha
Na Mwandishi wetu, Mirerani.  MKUU wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amewataka wachimbaji wa madini wa eneo hilo kuchangamkia bima ya afya kwa wote ili waweze kupatiwa huduma za matibabu pindi wakiugua.  RC Sendiga ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa chama wachimbaji cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara MAREMA uliofanyika kwa muda wa siku mbili Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro.  Ameeleza kwamba wachimbaji madini wa mkoa huo wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo ya bima ya afya kwa wote. Amesema bima ya afya kwa wote unachangia shilingi 150,000 kwa mwaka na unapatiwa huduma za afya kwa kaya ya watu sita wakiwemo baba, mama na watoto wanne.  "Wachimbaji madini mnapaswa kuchangamkia hii fursa kwani unakuwa na uhakika wa kupata matibabu wewe na familia yako pindi mkihitaji huduma na hamtapungukiwa na kitu na kununiana kutaisha," amesema RC Sendiga. Ameeleza kwamba hivi sasa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Ha...

MAREMA WAOMBA GETI LA TANZANITE KUWA WAZI SAA 24

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani.  WACHIMBAJI wa madini ya Tanzanite mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wameiomba serikali kuruhusu lango la kuingia na kutoka ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite kuwa wazi saa 24 ili shughuli zao zifanyike vyema. Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Manyara, (MAREMA) Elisha Nelson Mnyawi ameyasema hayo mbele ya mkuu wa moa huo Queen Sendiga kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho uliofanyika mji mdogo wa Mirerani.  Mnyawi ameeleza kwamba changamoto ya lango la kuingia na kutoka ndani ya ukuta kufungwa saa 5 usiku inawakwaza wachimbaji madini ya Tanzanite. Amesema endapo lango hilo likiwa wazi saa 24 kwa siku itakuwa vyema kwani shughuli za kiuchumi zitakuwa zimeboreshwa zaidi. "Tunavipongeza vyombo vya ulinzi na usalama ndani ya ukuta kwani wanafanya kazi nzuri ila wachimbaji wangepewa fursa ya lango hilo kuwa wazi saa 24 itakuwa bora zaidi kwao," amesema Mnyawi. Amesema endapo suala...